HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, November 23, 2014

TASWIRA MBALI MBALI KATIKA MAHAFALI YA TISA YA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE DAR ES SALAAM

Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Angellah Kairuki (kushoto), akimkabidhi cheti Muhitimu aliyefanya vizuri Shahada ya Kwanza ya Jinsia na Maendeleo, Nyamambara Simon katika Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere yaliyofanyika Dar es Salaam leo. W apili kulia ni Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo, Samwel Lunyelele na Mkuu wa Chuo, Profesa Shadrack Mwakalila.
 Wimbo wa Taifa ukiimbwa- Kutoka kulia ni Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo, Samwel Lunyelele na Mkuu wa Chuo, Profesa Shadrack Mwakalila, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuki, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Maryam Abdallah Yusuph na Mjumbe wa Bodi Dk.Terezya Huvisa (MB).
 Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Maryam Abdallah Yusuph, akizungumza katika mahafali hayo.
 Vyeti vikiendelea kutolewa.
 Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Mwanahabari, Msuya Selemani (katikati), akiwa na wanafunzi wenzake baada ya kuhitimu Shahada ya Kwanza ya Siasa na Uendeshaji wa Maendeleo ya Jamii. 
 Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Mwanahabari, Msuya Selemani , akiwa katika mahafali hayo
 Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema (wa pili kushoto), naye alikuwepo na waalikwa wengine.
 Ndugu jamaa na marafiki wa wahitimu hao wakiwa kwenye sherehe hizo.
 Ndugu wa wahitimu hao wakifuatilia matukio mbalimbali katika mahafali hayo.
 Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Mjumbe wa Bodi ya Chuo, Dk.Terezya Huvisa MB (kushoto), akitoa shukurani kabla ya kuhitimisha mahafali hayo.
 Wahitimu hawa wakitafakari jambo.
 Wageni waalikwa wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Blasi band ya Jeshi la Polisi ikitoa burudani.
 Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuku akiwaaga wageni waalikwa baada  ya kumalizika kwa mahafali hayo. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila.
Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuku akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu na viongozi wa chuo hicho.Picha na Doto Mwaibale wa Habari za Jamii Blog

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad