KIKUNDI cha Wanaume wapiga kasia cha Costantine Lusalage kutoka Sengerema Mkoani Mwanza
kimeibuka na ubingwa wa Mkoa wa fainali zakimkoa mbio za mitumbwi chini ya udhamini wa bia ya
Balimi Extra Lager zijulikazo kama “Balimi Boat Race 2014” na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi
900,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Mwanza kwenye fainali za Kanda zinazotarajiwa
kufanyika Desemba 6 mwaka huu jijini Mwanza.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha Elisha Jacob kutoka Misungwi ambacho kilizawadiwa pesa
taslimu Shilingi 700,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za Kanda jijini Mwanza pia,
wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha Emmanuel Masanyiwa kutoka Luchelele ambacho
kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 500,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Daniel Genha
kutoka Misungwi ambacho kilizawadiwa Shilingi 400,000/=.
Nafasi ya tano hadi ya tisa walipewa kifuta jasho cha pesa taslimu Shilingi 250,000/= kila kikundi
ambavyo ni kikundi cha Mussa Msalaba kutoka Sengerema, Joseph Jacob kutoka Misungwi, Katula
Msese kutoka Kigoto, Faustine Daud kutoka Ibanda, Lubongeja Manyasiwa kutoka Sengerema na Simon
Salala kutoka Misungwi.
Upande wa Wanawake kikundi cha Joyce Alon kutoka Misungwi kilifanikiwa kutwaa ubingwa na hivyo
kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 700,000/= pamoja na nafasi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za
Kanda jijini Mwanza.Nafasi ya pili Wanawake ilichukuliwa na kikundi cha Tabu Daudi kutoka Misungwi
ambao walizawadiwa Shilingi 600,000/=,washindi wa tatu ni kikundi cha Ntabo Hussein kutoka Luchelele
ambao walizawadiwa Shilingi 400,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Leah William
kutoka Misungwi ambao walizawadiwa Shilingi 300,000/= na nafasi ya tano hadi ya kumi walizawadiwa
kifuta jasho cha Shilingi 200,000/= kila kikundi ambavyo ni kikundi cha Winifrida William kutoka
Misungwi, Revina Magafu kutoka Kigoto, Anna Elias kutoka Kigoto, Moshi Maji ktoka Kigoto, Kizuka
Kapani kutoka Bwiru na Robby Mwita kutoka Mwaloni.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi Meneja wa bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa kwanza
alishukuru vikundi vyote vilivyojitokeza kushirika mashindano hayo lakini pia aliwapongeza wale wote
waliofanukiwa kupata zawadi na kuwaomba waliofanikiwa kupata nafasi ya kuwakilisha Mkoa wa
Mwanza kwenye fainali za Kanda wafanye mazoezi ya kutosha na mwisho wa siku ushindi wa ubaki
Mwanza kwa mwaka 2014.
Edith alisema washiriki wote mliofanikiwa kupata zawadi mkatumie vizuri hizo pesa kwa maendeleo
yeno na pamoja na maadalizi ya mashindano mengine mwaka ujao.
Fainali za Kanda za mbio za mitumbwi zijulikanazo kama “Balimi Boat Race 2014” zinatarajiwa kufanyika
Desemba 6, mwaka huu jijini Mwanza katika ufukwe wa Mwaloni.
Baadhi ya Wakimbia mbio za Makasia Wanaume wakichuana wakati wa fainali za mbio za Mitumbwi zinazodhaminiswa na Bia ya Balimi Extra Lager zijulikanazo kama “ Balimi Boat Race 2014” Mkoa wa Mwanza zilizofanyika mwishoni mwa wiki ambapo kikundi cha Costantine Lusalage kutoka Sengerema kilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mkoa upande wa Wanaume.
Wakimbia mbio za Makasia Wanaume wakiendelea kuchuana wakati wa fainali za mbio za Mitumbwi zinazodhaminiswa na Bia ya Balimi Extra Lager zijulikanazo kama “ Balimi Boat Race 2014” Mkoa wa Mwanza.
Baadhi ya Wakimbia mbio za Makasia Wanawake wakichuana wakati wa fainali za mbio za Mitumbwi zinazodhaminiswa na Bia ya Balimi Extra Lager zijulikanazo kama “ Balimi Boat Race 2014” Mkoa wa Mwanza zilizofanyika mwishoni mwa wiki ambapo kikundi cha Joyce Alon kutoka Misungwi kilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mkoa upande wa Wanawake.
Meneja wa bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa(kulia) akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa mbio la Mitumbwi zilizodhaminiwa na bia hiyo zilizofanyika Mwanza mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Meneja Masoka wa TBL Kanda ya Ziwa, Malaki Sitaki.
Washindi wa kwanza Wanawake wa mbio za Mitumbwi, kikundi Joyce Alon kutoka Misungwi Mkoa wa Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa kitita cha pesa taslimu Shilingi 700,000/= pamoja na nafasi ya kuwakilisha Mkoa wa Mwanza katika fainali za Kanda zinazotarajiwa kufanyika Mkoani humo Desemba 6,2014.
Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Ilemela, akimkabidhi Nahodha wa kikundi cha Constatine Lusalage kutoka Sengerema Mkoani Mwanza pesa taslimu Shilingi 900,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za Kanda mara baada ya kuibuka mabingwa wa mkoa wa mbio hizo za makasia zilizofanyika mwishoni mwa wiki Mkoani humo.
Washindi wa kwanza Wanaume wa mbio za Mitumbwi, kikundi Costantine Lusalage kutoka Sengerema Mkoa wa Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa kitita cha pesa taslimu Shilingi 900,000/= pamoja na nafasi ya kuwakilisha Mkoa wa Mwanza katika fainali za Kanda zinazotarajiwa kufanyika Mkoani humo Desemba 6,2014.
No comments:
Post a Comment