HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 30, 2014

Rais wa Zanzibar,Dkt Shein atembelea Benki ya Damu Salama

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifutana na Meneja wa  Kituo cha Damu Salama Dk.Mwanaheri Mahmoud Ahmed (kushoto) baada kutembelea chuma maalkum cha kuhifadhi Damu Salama iliyochangiwa na wananchi Mbali mbali  huko Sebleni Nyumba za Wazee Mjini Zanzibar leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiangalia Damu Salama zilizohifadhiwa katika mashine maalum akiwa na Aaza Humud katika chumba maalum alipotembelea katika Ofisi za Kituo hicho Sebleni Nyumba za Wazee Mjini Zanzibar leo
 Mkuu wa maabara ya kuchunguza maradhi mbali mbali Msafiri L.Marijani  akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) wakati alipotembelea Maabara katika Hospitali ya Mnazi mmoja leo Mjini Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa Kituo cha Damu Salama kiliopo Sebleni Nyumba za Wazee Mjini Zanzibar leo alipofanya ziara fupi kituoni hapo
 Afisa Mhamasishaji wa Kituo cha Damu Salama Omar Said Omar (kulia) akitoa mchango wake wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipozungumza na wafanyakazi  wa kituo hicho alipofanya ziara maalum ya kutembelea kuangalia maendeleo ya utendaji kazi Sebleni Nyumba za Wazee Mjini Zanzibar leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad