HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 2, 2014

ORIFLAME TANZANIA YATOA AJIRA KWA VIJANA 60,000 NCHINI - YATANGAZA BIDHAA ZAKE MPYA

Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Oriflame Tanzania inayouza vipodozi asilia imetoa ajira kwa vijana 60,000 wa kitanzania kwa kusambaza na kuuza bidhaa zake.


Hayo yalibainishwa na Meneja Mkazi wa Oriflame Tanzania, Fortunata Nkya wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo katika hafla ya kutangaza bidhaa mpya na uzinduzi wa kitabu chenye bidhaa mbalimbali za urembo kiitwacho Your Dreams-Our Inspiration kitakacho kuwa sokoni kuanzia  Oktoba 1 hadi Desemba 31-2014.



"Tangu tuanzishe kampuni hii mwaka 2011 tumefanikiwa kutoa ajira kwa vijana 60,000 jambo ambalo tunajivunia ukizingatia changamoto kubwa ya uhaba wa ajira" alisema Nkya.


Alisema vijana hao wamekuwa wakijipatia zaidi ya sh. milioni 10 kwa mwezi kutokana na kufanya biashara ya bidhaa zetu kwa mfumo wa moja kwa moja.


Nkya alisema kampuni yenye makao yake makuu nchini Sweden  kila baada ya miezi mitatu  inaingiza bidhaa mpya sokoni ili kutoa fursa kwa wateja wao kuzipata kwa urahisi na kuzisambaza kila kona kupitia mtandao wa vijana waliopo katika makundi.


Aliongeza kuwa bidhaa nyingi ni vipodozi asilia vinavyotumika kwa wanaume na vingi zaidi ni kwa ajili ya wanawake.


Nkya alitumia nadfasi hiyo kuwahamasisha wanawake kote nchini kununua vipodozi kutoka Oriflame Tanzania kwani havina kemikali yoyote ni bora na salama kwa mtumiaji kwa wakati wote.



Meneja huyo mkazi alisema kama atahijai ufafanuzi kuhusu namna ya kuzipata bidhaa zao anaweza kufika katika ofisi ya Oriflame iliyopo ghorofa la Benjamin William Mkapa Towers Mezzanine Floor.
Mkurugenzi Mwandamizi wa Kampuni Oriflame Tanzania, Japhet Naftal (kulia), akiwapigisha makofi wanachama wa Oriflame baada ya kuzungumza nao katika hafla hiyo ya kutangaza bidhaa mpya za Kampuni hiyo iliyofanyika katika ofisi zao Dar es Salaam leo jioni zilizopo Posta Mpya ghorofa la Benjamin William Mkapa Towers Mezzanine Floor..
 Meneja Mkazi wa Oriflame Tanzania, Fortunata Nkya (kulia), akizungumza na wanachama wa kampuni hiyo kuhusu bidhaa mpya na mipango ya miezi mitatu ya kampuni hiyo. Moja ya bidhaa mpya iliyonadiwa na kutangazwa ni The One Make -Up sanjari na kuzindua kitabu chenye bidhaa mbalimbali za urembo kiitwacho Your Dreams-Our Inspiration kitakacho kuwa sokoni kuanzia leo  Oktoba 1 hadi Desemba 31-2014.
 Viongozi wa Kampuni hiyo wakitambulishwa kwa wanachama. Kutoka kushoto ni Jesca Nisege, Meshack Wayanje, Julieth Msofe, Clara Wekwe, Christina Basil, James Mwangamba na Nasra Mohamed.
 Wanachama wa Oriflame Tanzania wakimsikiliza kwa makini Meneja Mkazi, Fortunata Nkya wakati akielezea mambo mbalimbali ya kampuni hiyo.
 Wanachama wa Oriflame Tanzania wakimsikiliza kwa makini Meneja Mkazi, Fortunata Nkya wakati akielezea mambo mbalimbali ya kampuni hiyo.
 Warembo wa Oriflame wakiwa katika sura ng'avu baada ya kutumia vipodozi vinavyosambazwa na kampuni hiyo hakika wanapendeza,  wakina mama nunueni vipodozi vya Oriflame ili mpendeze kama akina dada hawa. Kutoka kushoto ni mrembo Monica Mhando, Zainabu Ali na Suhaila Abdallah.
 Ofisa Mwandamizi wa Oriflame Tanzania, James Mwangamba akihojiwa na wanahabari hapo anaelezea mafanikio makubwa yaliyofikiwa na kampuni hiyo.
Wanachama wa Oriflame wakishangilia katika hafla hiyo.Imeandaliwa na Dotto Mwaibale wa Habari za Jamii Blog.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad