HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 1, 2014

DALADALA YAPARAMIA KIPITA SHOTO CHA YMCA, MOSHI

Gari aina ya Toyota Hiace linalofanya safari yake kati ya KCMC na katikati ya mji wa Moshi likiwa katika bustani ya mzunguko wa YMCA baada ya kupitiliza toka barabarani.
Sehemu ya uharibifu uliofanyika baada ya gari hilo kufeli breki na kunyoosha moja kwa moja na kugonga kingo za keep left ya YMCA.
Askari wa Kikosi cha usalama barabarani wakijaribu kuangalia maeneo yaliyoaharibika baada ya gari hilo kupita katika kipita shoto hicho.
Fundi mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja akitizama chini ya gari ili kutambua endapo kuna tatizo zaidi baada ya ajali hiyo ambayo hata hivyo haikusababisha madhara makubwa kwa abiria.
"Ni kama limeegeshwa "
Mahala ambapo magari yanaonekana kwa mbali ndiko daladala hii ilikuwa ikitokea na hatimaye ikashindwa kukata kuzunguka Kipita shoto ,dereva akaamua kufupisha Root kwa kukatiza katikati ya kipita shoto.
Mfuniko wa Chemba hii ni sehemu ambazo zimeathirika na ajali hiyo.

Mmhoa wa watumishi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi,akijaribu kuokoa vitu ambavyo vilikuwa katika Chemba hiyo kwa ajili ya kuvitafutia hifadhi nyingine.


Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad