HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 22, 2014

Chuo Kikuu Ardhi kutatua tatizo la udhibiti wa maji taka na taka ngumu

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi Prof. Idrissa Mshoro akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu mpango wa chuo hicho wa kuendelea na jitihada za kutatua tatizo la udhibiti wa maji taka na tanga ngumu ikiwemo ujengaji wa miundombinu ya majaribio ya teknolojia za kibiolojia zinazobadili tanga ngumu au maji taka ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji na gesi asili ya kupikia, wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma wa chuo hicho Prof. Gabriel Kassenga.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi ambaye pia ndiye mtaalam wa teknolojia za kibiolojia zinazobadili tanga ngumu au maji taka (waste treatment facilities) Dkt. Shabaan Mgana Akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) namna Teknolojia hiyo ya kubadili taka ngumu na maji taka inavyotumika na kuwasaidia wananchi walioonesha nia ya kuitumia ikiwamo kupata mboji kwa ajili ya mazao, mimea pamoja na kupata gesi asili ya kupikia, ambapo mpaka sasa kiasi cha nyumba 100 za awali katika mtaa wa Migombani, kata ya Segerea na nyumba mia moja katika Chuo Kikuu cha Ardhi zimeshaunganishwa katika Mradi huo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Idrissa Mshoro.
Mkemia Mkuu wa Kiwanda cha Mansoor Daya Chemicals Bw. Benedict Mtenga Akiwaeleza waandishi wa habari(hawapo pichani) jinsi wanavyoendelea kunufaika na teknolojia hiyo ya kibiolojia ikiwemo kutumika kusafisha maji taka yanayozalishwa na kiwanda hicho na kuepusha uharibifu wa mazingira,wakati wa ziara iliyofanywa katika kiwanda hicho ili kuona jinsi teknolojia inavyofanya kazi.
Miundombinu ya majaribio ya teknolojia za kibiolojia zinazobadili tanga ngumu au maji taka ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji zilizojengwa katika maeneo ya Chuo Kikuu cha Ardhi, mtaa wa Migombani, kata ya Segerea na katika kiwanda cha Madawa ya Binadamu cha Mansoor Daya Chemicals.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo na kutembelea maeneo ilipojengwa miundombinu ya teknolojia za kibiolojia zinazobadili taka ngumu au maji taka ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi Bi. Minza Selele akiwaeleza waandishi wa habari jinsi mtambo wa kuzalisha gesi asili inayotokana na mabaki ya chakula, taka za jikoni na mbogamboga, wakati wa ziara iliyofanywa chuoni hapo kujionea jinsi teknolojia ya kubadili taka ngumu na kuzalisha gesi asili ya kupikia inayofanya kazi.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi Bi. Minza Selele akiwasha karatasi kwa kutumia Gesi Asili iliyozalishwa na Mtambo huo. Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad