HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 16, 2014

TASWIRA ZA ADHA YA MVUA ENEO LA POSTA MPYA JIJINI DAR LEO

Wananchi wa maeneo mbali mbali ya jiji la Dar leo wamekumbana tena na adha ya mvua kubwa iliyopelekea eneo la Posta Mpya kujaa maji. 

Eneo hilo ambalo lipo mkabala na Benki ya Posta kwa muda mrefu limekuwa likijaa maji kutokana na mitaro ya Barabara ya Azikiwe kuziba lakini wahusika ambao ni Halmashauri ya Manispaa Ilala inaonesha wameshindwa kulimaliza hivyo kuleta usumbufu kwa watu wanatumia barabara hiyo pamoja na magari.
Wananchi wakipita kwenye dimbwi la maji maeneo ya Posta Mpya
Kijana akipita kwenye dimbwi hilo huku akisukuma tolori lake lenye madumu.
Maji yakiwa yameeneo katikaeneo hilo karibu na kituo cha kuuzia mafuta .
Kijana akipita kwenye dimbwi hilo mbele ya maegesho ya Tax katika eneo hilo.
Mwendesha baiskeli ya magurudumu matatu akipita eneo hilo. (Picha na mtandao wa habari za jamii.com)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad