HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 19, 2014

Tanzania, Thailand kushirikiana katika madini na vito

Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo (mwenye shati la batiki), akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito wa Thailand, walipotembelea Banda la Tanzania katika Maonesho ya 54 ya Vito na Usonara ya Bangkok, yaliyofanyika Septemba 9 hadi 13 mwaka huu.
Makamu wa kwanza wa Rais wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito na Usonara wa Thailand, Bw. Sutipong Dumrongsakul, akimkabidhi zawadi maalumu Mkuu wa Ujumbe kutoka Tanzania ulioshiriki maonesho ya vito ya Bangkok, Archard Kalugendo, mara baada ya kikao kati ya Ujumbe huo na Viongozi wa Taasisi hiyo ya Wafanyabiashara wa Thailand.
Wateja mbalimbali wakihudumiwa katika Banda la Tanzania kwenye maonesho ya vito na usonara ya Bangkok yaliyofanyika hivi karibuni nchini   Thailand.
Baadhi ya Watanzania walioshiriki maonesho ya vito na usonara nchini Thailand, wakimsikiliza mmoja wa wateja aliyetembelea Banda la Tanzania.
Ujumbe wa Tanzania (Kulia) wakiwa katika kikao na Uongozi wa juu wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito na Usonara wa Thailand, ambao ndiyo waandaaji wa maonesho ya vito na usonara ya Bangkok.
Baadhi ya Watanzania walioshiriki maonesho ya vito na usonara ya Bangkok, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungwa rasmi kwa maonesho hayo.
Makamu wa Rais wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito – Thailand, ambao ndiyo waandaaji wa Maonesho ya Vito ya Bangkok, Tony Brooke akizungumza na baadhi ya Watanzania walioshiriki katika Maonesho hayo nchini Thailand alipotembelea Banda la Tanzania. Sambamba naye (mwenye shati la kitenge) ni Mkuu wa Ujumbe wa Tanzania katika maonesho hayo, Archard Kalugendo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad