HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 23, 2014

NCHI ZA ME ZAWEKEZA ZAIDI KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA UHALIFU MTANDAO

 Ukipitia takwimu za mwaka huu na mwaka jana inaonyesha Nchi za Ulaya na Marekani zimeendelea kuathirika zaidi na uhalifu mtandao, Huku Nchi za mashariki ya kati kuonekana kunyemelewa na wahalifu mtandao. Wakati huo huo takwimu zilitabiria Nchi za Afrika  kuwa katika hali mbaya baadae kutokana na ukuaji wa kasi wa matumizi ya mitandao ambao hauendani sanjari na maandalizi madhubuti ya usalama wa mitandao.

Mengi yalizungumzwa kuhusiana na tishio jipya katika nchi za kiarabu huku kampuni inayojihusisha na ulinzi mtandao ya Kaspersky wakiandika "NCHI YA SAUDI ARABIA" imedhamiriwa zaidi na wahalifu mtandao kauli ambayo iliambatana na "UTAFITI" ukibainisha kampuni za mashariki ya kati zimeendelea kulengwa na wahalifu mtandao.

Hatua hiyo ilisababisha nchi hizo za mashariki ya kati kuwekeza zaidi na kuimarisha jitihada zake za mapambano dhidi ya uhalifu mtandao. "JEDDAH" iliyoko Saudi Arabia ilianzisha kituo kipya kilicho imarishwa maalum kwa ajili ya mapambano dhidi ya uhalifu mtandao na Hivi karibuni "JORDAN" nao wakazindua kituo chao maalum kwa ajili ya kupambana na uhalifu mtandao.

Vile vile nchi nyingine za Mashariki ya kati (ME) zimeendelea kuwekeza na kufungua vituo maalum kwa ajili ya mapambano dhidi ya uhalifu mtandao katika ukanda huo ambapo imeenda sambamba na uboeshwaji wa sharia mitandao.

NINI TUNAJIFUNZA KAMA TAIFA?

Tayari imezoeleka nchi za ulaya na Marekani zimekua vinara kwenye kuwekeza katika mapambano dhidi ya uhalifu mtandao kutokana na athari kubwa ambayo tayari imesha ziona.Na hivi sasa inaonekana Nchi za Mashariki ya kati nazo zikiwekeza katika upande huo. 


Nchi za Afrika pia zimeendelea kujipanga na kkuwekeza kwenye sekta hii ambayo inaonekana kuwa tishiokubwa mapema baadae. Jitihada zilizopo zinapaswa kuendana sambamba na kuweka vizuri sharia mtandao huku itafutwa njia rafiki itakayofungua mipaka kwenye mapambano dhidi ya uhalifu huu mtandao ambao hauna Mipaka.


Maboresho ya mara kwa mara yanahitajika kwenye vituo maalum vya mapambano dhidi ya uhalifu mtandao pamoja na kuwa na mapitio ya sheria mtandao mara kwa mara kutokana na mabadiliko na ukuaji wa teknolojia inayochangia kasi ya uhalifu mtandao kuongezeka. Haya na mengine nimepata kuya ainisha  kwa kina kwenye andiko linaloweza kusomeka "HAPA"

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad