HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 30, 2014

MAAFISA KUTOKA AFRIKA KUSINI WATEMBELEA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Na Veronica Simba – Dar es Salaam

Maafisa Wakuu 35 kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Afrika Kusini (South African National Defence College – NDC), wametembelea Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini Septemba 30, 2014 kwa lengo la kujifunza kuhusu Sera ya Tanzania kuhusu vyanzo vya nishati nchini hususan mafuta, gesi, makaa ya mawe na uvumbuzi wa madini mengine na changamoto zake.

Maafisa hao waliongozwa na Mkuu wa Chuo Brigedia Jenerali G.M. Yekelo pamoja na Maafisa kutoka jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao ndiyo wenyeji wa wageni hao hapa nchini.

Wakiwa Wizarani, Maafisa hao walipokelewa na Viongozi na Maafisa Waandamizi wa Idara za Nishati na Madini na kupewa maelezo mafupi kuhusu vyanzo vya nishati nchini pamoja na rasilimali za madini.

Ujumbe huo upo nchini kuanzia Septemba 27 kwa ziara ya mafunzo na wanatarajia kurejea Afrika Kusini Oktoba 2, 2014.
Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Afrika Kusini (South African National Defense College – NDC), Brigedia Jenerali G.M. Yekelo akiuliza swali kuhusu rasilimali ya gesi asili kwa Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mhandisi Nobert Kahyoza (wa kwanza kushoto).
Mmoja wa Maafisa kutoka Chuo cha NDC akitoa salamu za shukrani kwa Wizara ya Nishati na Madini kwa niaba ya wenzake.
Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mhandisi Nobert Kahyoza (kushoto), akipeana mkono na mmoja wa Maafisa kutoka NDC, baada ya kukabidhiwa zawadi kwa niaba ya Wizara ya Nishati na Madini.
Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mhandisi Nobert Kahyoza akitoa maelezo kuhusu Kitabu chenye kueleza rasilimali za madini yaliyopo Tanzania kabla ya kukikabidhi kama zawadi kwa Ujumbe wa Maafisa wa NDC.
Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mhandisi Nobert Kahyoza akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wizara ya Nishati na Madini kwa Ujumbe wa Maafisa kutoka NDC waliofika kutembelea Wizarani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad