HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 1, 2014

BODI YA WAKURUNGENZI YA DAWASA YATEMBELEA ENEO LA MRADI WA UJENZI WA BWAWA LA MAJI KIDUNDA

Meneja Usimamizi, Undeshaji na Mazingira toka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaama (DAWASA), Bi.Modesta Mushi akiwaneosha Wajumbe wa Bodi ya Wakurungenzi wa mamlaka hiyo ramani ya Ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Kidunda lenye ujazo wa Mita milioni 190, Agosti 29, 2014 wakati wa ziara ya Bodi hiyo katika eneo la Mradi Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Timu ya Ulipaji fidia kwa Wakazi walio katika Eneo la Mradi, Mhandisi. John Kirecha akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurungenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), kuhusiana kukamilika kwa taratibu za ulipaji fidia kwa wakazi waliopisha ujenzi wa mradi wa bwawa la Kidunda litakaloweza kutoa huduma kwa mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro, wakati wa Ziara ya hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Bw. Archard Mtalemwa akisisitiza jambo.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Alhaji Said El-Maamry (kulia), akimuuliza swali Mhandisi. John Kirecha kuhusiana fidia kwa Wakazi walio katika Eneo la Mradi huo, likiwemo kuhakikisha taratibu hizo haziathiri maendeleo ya ujenzi wa huo.
Mkuu wa Timu ya Ulipaji fidia kwa Wakazi walio katika Eneo la Mradi, Mhandisi. John Kirecha akitoa maelezo kuhusiana na taratibu za ulipaji fidia kwa wananchi hao.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Alhaji Said El-Maamry (kushoto), pamoja na Wajumbe wa Bodi hiyo wakimsikiliza kwa umakini Mhandisi. John Kirecha wakati akitoa maelezo kuhusiana ulipaji fidia kwa wakazi waliopisha ujenzi wa mradi wa bwawa la Kidunda litakaloweza kutoa huduma kwa mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro, wakati wa Ziara ya hiyo.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurungenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), wakiondoka mara baada ya kutembelea, kujione namna taratibu zinazofanyika za ulipaji fidia kwa wakazi hao.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurungenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), wakiwasili katika eneo la Bwira juu lililotengwa kwa ajili ya makazi mapya kwa wakazi waliopisha ujenzi wa Mradi huo.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurungenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), wakiangalia Ramani ya Viwanja 1000 vilivyopimwa vya Makazi mapya viliovyoko eneo la Bwira juu kwa wakazi wapatao 2068 waliopisha Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Kidunda.
Msimamizi wa Kitengo cha Usimamizi na Upimaji Ramani wa Wilaya Mkoani Morogoro, Bw.Kitomanga Francis (alievaa Kaunda suti), akitoa maelezo mbele ya Wajumbe hao juu ya matumizi ya viwanja likiwemo ujenzi wa shule, makazi, Hospitali, Kituo cha Polisi,pamoja na huduma nyingine muhimu.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Bw. Alhaji Said El-Maamry (mwenye tisheti), Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Bw. Archard Mtalemwa (mwenye shati jeupe), wakijadiliana jambo wengine ni Wajumbe wa Bodi ya Wakurungenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), katika eneo la Bwira juu mara baada ya kutembelea, lililotengwa kwa ajili ya makazi mapya kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Mradi huo. PICHA NA PHILEMON SOLOMON

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad