HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 22, 2014

MH. PINDA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA JAJI MAKAME

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimian na Mawaziri Wakuu, Wastaafu, Frederick Sumaye na Jaji Joseph Warioba (wapili kulia) kabla ya kuzungumza kwa niaba ya serikali na kutoa heshima za mwisho kwa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, marehemu Jaji Lewis Makame kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam August 22, 2014. Kulia nI jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na jaji Mkuu Mohamed Chande Othman (kulia) na Mawaziri Wakuu Wastaafu, Joseph Warioba (wapili kulia) na Frederick Sumaye kabla ya kutoa salamu za Serikali na heshima za mwisho kwa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, marehemu Jaji Lewis Makame kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam August 22, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole Jaji Leila Makame Mgonya mmoja wa wana familia, wa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Marehemu Jaji Lewis Makame baada ya kuzungumza kwa niaba ya serikali na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu huyo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam August 22, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Marehemu Jaji Lewis Makame baada ya kuzungumza kwa niaba ya serikali kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam August 22, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Jeneza lenye mwili wa Marehemu aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame likiwa mbele ya viongozi wa Serikali, ndugu, jamaa na marafiki kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda akisaini kitabu cha maombolezo wakati wa kuuaga mwili wa Marehemu aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali wa Serikali wakilisikiza wasifu wa marehemu aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Ndugu, jamaa na marafiki wakiwa na nyuso za uzuni wakati wa kuuaga mwili wa Marehemu aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wafiwa akilia kwa uchungu wakati akiuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad