HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 21, 2014

demo-image

KAMPUNI YA TANZANIA DISTILLERIES LTD (TDL) YAZINDUA KINYWAJI KIPYA CHA KIMATAIFA, FYFE'S SCOTCH WHISKY KATIKA SOKO LA TANZANIA

KAMPUNI ya Tanzania Distilleries Ltd (TDL) imeendelea kujitanua katika soko nchini baada ya kuzindua kinywaji kipya cha kimataifa kiitwacho Fyfe's Scotch Whisky.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kinywaji hicho Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwassa alisema Fyfe's ni kinywaji maridhawa kinachoandaliwa kikamilifu kikiwa na radha murua na ya kipee.

"Ubora wa kinywaji hiki unatokana na umahiri mkubwa wa waandaaji na pia unatokana kimea na nafaka bora zilizotumika na kuwa Fyfe's Whisky huvundikwa kwa miaka kadhaa katika mji Loch Lomond, Scotland ili kuongeza ubora wake kabla ya kuwa tayari kwa matumizi" alisema Mgwassa.

Mgwasa aliongeza kuwa kampuni yao imekuwa ikiwaletea watanzania vinywaji mbalimbali ambavyo vimekuwa chachu katika kusherehekea hatua tofauti za mafanikio yao na kuendelea kuwaletea ladha tofauti za vinywaji bora.

Alisema kinywaji hicho ni zawadi ya pekee katika soko na kuwa Tanzania imekuwa nchi ya kwanza ulimwenguni kuzinduliwa na baadaye kitazinduliwa nje nyingine.
2
Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwassa, akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa kinywaji hicho.
3
Langa Khanyile akitoa ufafanuzi wa Whisky hiyo kabla ya uzinduzi.
4
Sehemu ulipo fanyika uzinduzi huo katika Hoteli ya Serena.
5
Wadau mbalimbali wakigongesha glasi zenye Whisky hiyo wakati wa hafla hiyo.
7
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd (TDL), David Mgwassa (wa pli kushoto), akiwa na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa kinywaji kipya kiitwacho Fyfe’s Scotch whisky, iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Kushila Thomas.
8
Wageni waalikwa wakigongesha glasi lenye kinywaji hicho.
DSC_2922
DSC_2924
Wasanii wakitoa burudani kwenye hafla hiyo.
DSC_2938
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo huku wakipata kinywaji hicho.
DSC_2939
Hapa kinywaji hicho kikipitishwa kwa wageni waalikwa.
DSC_2941
Wadau wakiwa kwenye hafla hiyo.
DSC_2948
Hapa wadau wakinywa na kugongesha glasi za whisky hiyo
DSC_2969
Mdau Ngobile Ngwenya akionesha kinywaji hicho.
DSC_2973
Hapa wanamuziki wakitoa burudani.

DSC_2995
Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwassa (kulia), akimkabidhi tiketi ya kwenda nchini Scotland, Mshindi wa bahati nasibu ya papo Benard Suma iliyotolewa na TDL.
DSC_2996
Mshereheshaji wa hafla hiyo Jimmy Kabwe (katikati), akizungumza na mshindi huyo Benard Suma jinsi anavyojisia baada ya kushinda. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwassa.Picha zote na Dotto Mwaibale.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *