HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 29, 2014

JOPO LA MAJAJI LA KUMTAFUTA MSHINDI WA TUZO YA RAIS YA HUDUMA ZA JAMII NA UWEZESHAJI YAENDELEA NA ZOEZI LAKE JIJINI TANGA NA WILAYA YA MKINGA

Majaji Bw. Venance Bahati (kushoto) na Bi. Costansia Gabusa (kulia) wakijadiliana jambo wakati wa kufanya tathmini ya mradi wa ukingo uliojengwa pembezoni mwa bahari kwa ajili ya kuzuia mmomonyoko katika eneo la Mwarongo jijini Tanga. Ukingo huo umejengwa kwa msaada wa kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Tongoni Bw. Mzihili Abeid (kushoto) akitoa maelezo mbele ya majaji waliotembelea maabara ya shule hiyo. Maabara hiyo imejengwa na kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC.
Msimamizi wa kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC Bw. Ahmed Omar (kulia) akizungumza na jopo la majaji na sektretarieti kwenye maabara ya shule ya sekondari ya Tongoni iliyofadhiliwa na kampuni hiyo.
Jaji Venance Bahati (katikati) akiteta jambo na msimamizi wa kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC Bw. Ahmed Omar (kulia). Kushoto ni Jaji Costansia Gabusa.
Msimamizi wa kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC Bw. Ahmed Omar (kushoto) akizungumza na majaji walipotembelea maabara ya Shule ya Sekondari ya Mabokweni jijini Tanga ambapo kwa sasa kampuni hiyo imejitolea kuwajengea maabara ya kisasa.
Mkurugenzi wa kampuni ya Dawson Food Products Ltd iliyopo wilayani Mkinga mkoani Tanga Bw. Burhani Taibali (kulia) akizungumza na majaji pamoja na sekretarieti iliyotembelea kampuni hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad