HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 28, 2014

CHINA YAIMWAGIA MISAADA JESHI LA POLISI, NAIBU WAZIRI SILIMA ATOA PONGEZI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akiiwasha moja ya pikipiki zilizotolewa na Serikali ya China kwa ajili ya kulisadia Jeshi la Polisi. Jumla ya pikipiki 50 zilitolewa na China ikiwa ni misaada yao ya mara kwa mara kwa ajili ya kulisadia jeshi hilo kwa lengo la kukabiliana na uhalifu nchini. Hata hivyo, Naibu Waziri Silima aliishukuru Serikali ya China kupitia Balozi wake nchini, Lu Youqing (wapili kushoto).
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kushoto) akimkabidhi Balozi wa China nchini, Lu Youqing zawadi ya ngao ambayo ina ujumbe wa kuishukuru Serikali yake kwa kutoa misaada mbalimbali kwa ajili ya kulisaidia Jeshi la Polisi nchini. Serikali hiyo ya China ilitoa misaada ya Pikipiki, Kompyuta na Samani za ofisini katika hafla fupi iliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo.
Balozi wa China nchini Tanzania, Lu Youqing (watatu kushoto) akimkabidhi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (wapili kushoto) msaada wa meza na viti kwa ajili ya kutumika katika ofisi za Jeshi la Polisi. Pia Serikali ya China ilitoa misaada ya Pikipiki na Kompyuta kwa ajili ya kulisaidia jeshi hilo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (katikati-waliokaa), Balozi wa China nchini, Lu Youqing (wapili kulia), Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Abdulrahman Omar Juma Kaniki (wapili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Serikali ya China imetoa misaada ya Pikipiki, Kompyuta na Samani za ofisini kwa ajili ya kulisadia Jeshi la Polisi. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad