Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na maelfu ya Waumini wa
Karismatiki Katoliki, Jimbo la Dar es Salaam katika maombi maalumu kwa ajili ya kuliombea
Taifa yaliyofanyika Kituo cha Karismatiki, Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Waziri Chikawe
ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo aliyataka Makanisa nchini kudumisha amani
na utulivu na kuendelea kuliombea Taifa na kuepuka kuingia katika migogoro mbalimbali
ambayo itasababisha taifa kuingia katika uvunjifu amani makanisani. Aidha, Chikawe aliongeza
kuwa migogoro katika Makanisa na Madhehebu mbalimbali nchini imekuwa mingi katika
kipindi hiki ambapo migogoro hiyo inasababishwa na ubinafsi wa viongozi, kutofuata Katiba
na Ubadhirifu wa mali za Kanisa. Kutokana na migogoro hiyo Chikawe alisema “Serikali
haitavumilia vitendo vya uvunjifu wa amani makanisani na ikibidi itafuta usajili wa madhehebu
na makanisa yenye migogoro ili kuepusha shari”.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto) akiungana na maelfu
ya Waumini wa Karismatiki Katoliki, Jimbo la Dar es Salaam katika maombi maalumu kwa
ajili ya kuliombea Taifa. Mapombi hayo yalifanyika katika Kituo cha Karismatiki, Ubungo
jijini Dar es Salaam leo. Waziri Chikawe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo
aliyataka Makanisa nchini kudumisha amani na utulivu na kuendelea kuliombea Taifa na
kuepuka kuingia katika migogoro mbalimbali ambayo itasababisha taifa kuingia katika uvunjifu
amani makanisani. Aidha, Chikawe aliongeza kuwa migogoro katika Makanisa na Madhehebu
mbalimbali nchini imekuwa mingi katika kipindi hiki ambapo migogoro hiyo inasababishwa na
ubinafsi wa viongozi, kutofuata Katiba na Ubadhirifu wa mali za Kanisa. Kutokana na migogoro
hiyo Chikawe alisema “Serikali haitavumilia vitendo vya uvunjifu wa amani makanisani na
ikibidi itafuta usajili wa madhehebu na makanisa yenye migogoro ili kuepusha shari”. Picha na
Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment