HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 25, 2014

Mamlaka ya maji safi Masasi yalia na wezi wa mita za maji

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira masasi-Nachingwea (MANAWASA) inatoa taarifa ya kusikitishwa kwake kutokana na matukio yasiyo ya kiustaharabu yanayoendelea hivi sasa ya wizi wa "MITA ZA MAJI" zilizofungwa na wateja kwenye maeneo wanayoishi ambapo mpaka sasa tayari mita 7 zimeshaibiwa na watu wasiojulikana kwenye mitaa ya MKUTI, JIDA pamoja na REST CAMP.

hivyo Mamlaka ya MANAWASA inawaomba wakazi wote wa mji wa masasi wenye nia njema na huduma hii muhimu kwa wananchi kutoa ushirikiano katika kuwafichua wezi hao na hatimaye wafikishwe mahakamani kwa hatua nyingine za kisheria. 

"EWE MKAZI WA MASASI KUMBUKA KWAMBA HAPO AWALI MASASI HAIKUWA HIVI ILIVYO SASA KWENYE SUALA LA MAJI" Hivyo ni vyema kila mmoja akawa mlinzi wa mwenzake ili kuifanya miundombinu ya MANAWASA iendelee kudumu wakati wote...

pia MANAWASA inatoa wito kwa wale wenye tabia ya kuchimba mchanga karibu na mabomba ya maji kwenye barabara kuu itokayo mtwara kuingia masasi waache mara moja kwani kwa kufanya hivyo husababisha mabomba hayo kupasuka na maji kushindwa kufika Masasi.
Baadhi ya miundombinu ya maji ya Mamlaka (MANAWASA).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad