HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 16, 2014

BAADA YA NEEMA YA MWENYEZI MUNGU KUTUSHUKIA LEO JIJINI DAR,HAKUNA HAJA YA KUCHUKIA ZAIDI YA KUFANYA HIVI

 Leo imeshesha mvua ya kama buku kadhaa hivi na kupelekea maeneo mengi ya jiji kuwa kama ionekanavyo pichani.hivyo hatuichukii hali hii na tunaendelea kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutushusia Neema hii.ila yatupasa tuendelee kumuomba Mwenyezi ili atupunguzie kidogo Neema hii.
Hapa ni mwendo wa viatu mkononi na kupiga mbizi tu.
 Fundi magari nae aliamua kuendelea kupiga spana juu ya maji.
 Mara spana imezama kwenye maji na akaanza kuisaka kinamna hii.
 Huduma ya kuweka na kutoa pesa kwa simu ilisamama kwenye duka hili maana hakuna mtu aliekuwa anaweza kufika katika eneo hilo.
 Hapa Dada nanihii nae mambo ndio kama yanavyoonekana hivyo kaamua kuketi na kuweka miguu juu.
 Vyombo vya Moto na watembea kwa Miguu leo wote walitumia njia moja.
 Biashara ya Dawa kwa ndugu zangu hawa iliingia ruba na sasa wanaondoka eneo la shughuli yao na kuelea nyumbani kupumzika.
 Braza nanihii nae alipofika hapa akasimama na kuanza kuwaza namna atakavyoimaliza safari yake kwenye maji hayo.
 Hakuna gari iliyoweza kutoka hapa.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad