HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 9, 2014

WATAALAM WA TEHAMA KATIKA NGAZI YA DUNIA WAKUTANA KUJADILI MASWALA MBALI MBALI

Mkutano Mkuu ulio washirikisha wataalam wa sekta ya teknologia katika ngazi ya kidunia umemalizika salama na kuna mengi ambayo yamepata kujadiliwa kwa kina .
Kwa kifupi yaliyojiri katika mkutano huo ni pamoja na :-

1.      Mapitio ya takwimu za makosa mtandao kwa kina katika mwaka huu. Mjadala ulibobea zaidi katika, nini hasa sababu ya makosa haya kuonekana kukua na nini kifanyike ili kupunguza kasi ya ukuwaji makosa haya.
2.      Namna ya utumaji wa “Key” ambazo zimetumika kuficha maneno “Encryption Key” ili kuweza kuongeza wigo wa usiri katika taarifa zinazo safirishwa kupitia mitandao.
3.      Hali halisi katika Teknologia mpya ya “CLOUD COMPUTING” na wasi wasi uliozuka juu ya usalama wa taarifa zinazopokea huduma kupitia teknologia hiyo. Pali jadiliwa kwa kina usahihi wa hilo na nini kifanyike.

4.      Mjadala wa kina kuhusiana na “Social media” na jinsi inavyoweza kusaidia kuelimisha jamii na kuleta mabadiliko chanya. Pia Namna ya kusaidia kuboresha na kuhimiza matumizi bora ya mitandao hiyo ya kijamii “Control mechanism to social media”4.      Changamoto zilizopo katika ukusanyaji na uchunguzi salama wa vidhibiti vya makosa ya Digitali “Digital forensics collections and investigations”.

5.      Mjadala wa kina katika matumizi ya Open source security info management (OSSIM) ambapo inatoa msaada mkubwa katika ulinzi wa mtandao ambapo mjadala huu ulifunguliwa na mhakiki mkuu “Chief editor” wa kitabu maarufu kinacho tumika sana katika ulinzi mtandao kiitwacho “Cyber security standard”.

6.      Mjadala Mwingine Kuhusiana na Teknologia Mpya ya Miwani ambayo inauwezo wa kuchukua taarifa kwa njia ya sauti na video na kuzisafirisha taarifa hizo kwenda sehemu nyingine. Tuliangali jinsi gani wa halifu sasa wameanza kuitumia vibaya teknolojia hiyo na umakini unahitajika kiasi gani.

7.      Mkuu wa MENA, alifafanua juu ya ukuaji wa teknologia kwa sasa na kusisitiza mafunzo ya mara kwa mara ili kwenda sambamba na ukuaji wa teknologia.

8.     Umuhimu wa kuelimisha jamii kua swala la ulinzi mtandao si jukumu la kundi Fulani bali ni jukumu la kila mmoja ilitumika kauli “ inaanza na wewe mimi na wengine wote, kwa pamoja tutaweza kupunguza hali mbaya ya makosa mtandao”

9. Aidha mjadala shirikishi kuhusiana na “Kifaa kipya kilichoko katika hatua za awali katika utafiti ambacho kitatumia teknologia kuweza kutoa tiba ya ugonjwa wa saratani “Cancer” ambacho kinategemea kupunguza madhara mengi yaliyopo kwa sasa ikiwemo kuondoa swala la mgojwa kunyolewa kipara.
Bwana Yusuph Kileo akiwa na Steven “FOUNDER” NA “CEO” wa Cloud perspectives (Cloud computing) Nje ya Ukumbi wa mkutano mara baada ya kumaliza sehemu ya kwanza ya kikao hicho.
Bwana Yusuph Kileo akiwa na Richard (mwenye miwani takikati) “Co-founder wa VENTURE na Mkuu wa The smart Cities – MENA”, CEO wa FZ – LLC Dr. Satti ( mwenye miwani wa kwanza kushoto) wakimsikiliza mwakilishi kutoka KSA alipokua akizungumzia kuhusiana na “Network security issues” katika chumba kidogo nje ya ukumbi wa mkutano mara baada ya chai ya asubuhi.
Bwana Yusuph Kileo kiwa na Dr. Ferguson (wa kwanza kulia) pamoja na Dr. Ebong ( wawakilishi kutokea North Caroline, USA. Dr. Ebong ndie anaeongoza hatua za awali katika utafiti wa kifaa kuhusiana na Saratani – Rejea namba 10.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad