HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 29, 2013

Taarifa Fupi Juu Ya Hali Ya Usalama wa kimtandao

Mr. Yusuph Kileo (Cyber Security and Digital 
forensics Investigations Expert)
Hivi karibuni kwa takriban miezi miwili kumekua na midahalo mbali mbali ambayo imekua ikiendelea katika nchi nyiingi na nimepata kuhudhuria kama mwanachama wa kudumu wa kikundi kinacho jihusisha na maswala ya Ulinzi mtandao katika nchi za Africa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyo wasilishwa na Profesa Hamadoun Toure kutoka ITU (International Telecommunication Union) iliyo chini ya United Nations (Umoja wa Kimataifa) ilisema kuna mategemeo mwishoni mwa mwaka huu wa 2013 pakawa na watumiaji biilioni 2.7 wa mtandao na kwa takwimu hizo zimeonyesha kupanda kwa kasi kulinganisha na takwimu za awali zilizotolewa mwishoni mwa mwaka jana katika mkutano ulio fanyika nchini afrika kusiini.Katika Vikao tofauti vilivyo kaliwa majadiliano yalikua ni mengi ambapo hali ya usalama wa kimtandao imechambuliwa kwa ngazi ya kidunia na kudhihirika ya kua kumekua na ongezeko kubwa katika mwaka huu wa 2013 la makosa mtandao, Hadi sasa nchi baadhi tayari zimeweza kupiga hatu katika kukabiliana na hali hiyo.

Aidha ripoti iliyowasiilishwa na ITU huko Geneva  ilisema, kumekua na ongezeko kubwa la madhara ya mtandao ambapo ilielezwa mitandao imekua ikiathiriwa zaidi kwa Asilimia 30, “Phishing Sites spoofing social networks” imeongezeka kwa asilimia 125 na kuelezwa nusu ya vijana wenye umri kati ya miaka 13 hadi 17 uliimwenguni kote wamekua wakiathirrika na kilichotambulishwa kama “Cyberbulling”.

Vile vile Tafiti zilizo wasilishwa katika ripoti ya “the World Federation of Exchanges and the
International Organization of Securities Commissions” 
zime eleza nusu ya taasis za fedha duniani zimeweza kuathirika na “Cyber-attacks” pamoja na wizi mtandao hadi kufikia mwaka jana mwishoni huku ikielezwa kushindikana kutatua hali hiyo kwa takriban robo nzima ya taasisi hizo za fedha dhidi ya tatizo hilo.

Hayo na mengine mengi ambayo yamepata kujadiliwa kwa kina yalionekana kuwa ni changamoto kubwa katika dunia ya sasa ambapo kutakua na ugumu sana kukimbia utumiaji wa teknologia katika maisha yetu yakila siku. Kwa sasa hali ya utumiaji wa mitandao kuongezeka nchini katika sekta mbali mbali kuanzia kufanya miamala ya biashara hadi katika sekta za elimu na maeneo mengine mengi.

Wimbi kubwa nchini limeongezeka la watu kuwa na matumizi mabaya ya mitandao ambapo imekua ikileta athari kubwa kwa jamii katika maeneo mengi hasa yaki biashara lakini pia hata kutishia hali ya usalama wanchi kwa kusambazwa maneno mbali mbali ya kutishia Amani ya nchi kwa kipindi kifupi tofauti na awali wakati matumizi ya mtandao hayakua na ongezeko lililoko sasa.

BOFYA READ MORE HAPO CHINI KUSHOTO KUSOMA ZAIDI
  

Ni kweli kila mtu hivi leo anahitaji teknologia ili kuweza kuwasiliana na mwingine, kufanya miamala ya kibiashara na hata kupata huduma mbali mbalii ambazo zimesogezwa karibu na wananchi kwa msaada wa mtandao, lakini pia kuna watu baadhi wanatumia fursa hiyo kufanya mambo yasiyo faa kupitia mitandao hiyo hiyo ambapo baadae inaweza kupelekea  usalama wa taifa letu kuingia dosari.

Profesa Hamadoun Toure katika taarifa yake ameeleza, ITU imeweza kueleza mafanikio ya jitihada kuubwa zilizo fanywa na nchi mbali mbali ambapo imepelekea Umoja wa Ulaya (EU) kuanzisha kilicho tambulishwa kama “Framework” katika ulinzi mtandao ambapo kila nchi mwana chama ameweza kunufaika katika hilo.
Kwa sasa ITU imeanzisha  “World’s First comprehensive alliance against cyber threats” ambapo nchi 145 zinapokea huduma hiyo kwa kuwaleta pamoja wadau mbali mbali wenye uuwezo wa kupambana na matishio ya kimtandao. 

Uhamasisho mkubwa umetolewa kwa serikkali mbali mbali, sekta binafsi pamoja na jumuia mbali mbali kuweza kulichukulia swala hili la makosa mtandao kwa sura ya kipekee ili kuweza kuunganisha nguvu ya pamoja kwa nchi zote duniani kuweza kukabiliana na tishio mtandao “Cyberthreats” ambapo baadae inaweza kugharimu dunia yetu ya leo.

Kwa sasa nchi ya Australia wametoa muongozo wa kutekeleza mbinu kuu nne(4) za kiusalama kwa mitandao ili kukabiliana na athari zinazoweza sababishwa na matatizo ya matumizi mabaya ya mitandao huku ikielezwa hatua hiyo itaweza kupunguza kwa asilimia 85 ya kuingiliwa kwa mitandao ya nchi hiyo.

Imefika wakati sasa na Tanzania kuiga mfano ya jitihada za nchi nyingine ili kuweza kuweka hali ya usalama mtandao nchini katika kiwango kizuri. Napenda kutoa sifa kwa  nchi kubwa kama China Urusi na Marekani kwa kuwekea mkazo maswala ya ulizi mtandao kwa kuazisha majadiliiano mbali mbali ikiwemo pia kufadhili majadiliano mbali mbali yanayo husiha maswala ya ulinzi mtandao.

Mbali namafanikio Kiasi ya Implementation ya Yaliyo patikana katika vikao vya awali sasa nipo katika hatua za awali kuifanyia kazi yale yaliyo patikana katika vikao mbali mbali vya hivi karibuni nikiwa kama mtaalam na mshauri katika maswala ya ulinzi mtandao na upelelezi/uchunguzi wa makosa ya digitali kwa kuanzia “Tanzania Crime Awareness campaign” na hasa nategemea kuangalia zaidi wenzetu katika nchi nyingine walipotilia mkazo ambapo ni katika makosa mtandao kwa hatua zaidi.

2 comments:

  1. Hali Ya Wizi Wa Kimtandao sasa imekua Tishio Balaa
    Sijui watu tuache kutumia Mitandao au tukimbilie wapi.

    ReplyDelete
  2. Ni kweli kwa sasa Hali ni mbaya Sana katika mitandao Ila Kumekua na Jitihada za Dhati kukabiliana na Hali hiyo na Soon Kutakua Na Updates Juu Ya mafanikio mengine katika Kuimarisha Hali ya Usalama Mtandao.
    Thanks For your Thoughts.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad