HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 1, 2013

uzinduzi wa usafi wa mazingira kwa wafanyakazi wa kampuni ya reli

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania-(TRL) Kipallo Kisamfu akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam kwa ajili ya uzindizi wa wiki ya mazingira kwa ngazi ya TRL uliofanyika katika Stesheni ya Dar es salaam . Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu upande wa Kampuni hiyo ni Fikiri kabla ya kula: hifadhi mazingira kwa uchukuzi endelevu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Reli Tanzania( TRL) Severine Kaombwe akiwahutubia wanyakazi wa Kampuni hiyo leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa wiki ya mazingira ngazi ya Kampuni nchini kote ambapo kauli mbiu yao ni Fikiri kabla ya kula: hifadhi mazingira kwa uchukuzi endelevu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Reli Tanzania( TRL) Severine Kaombwe akionyesha baadhi ya stika ambazo zitabandikwa katika Mabehewa mbalimbali kwa ajili ya uhamasishaji wa utunzaji mazingira kwa abiria wawapo ndani ya treni . Mwenyekiti alionyesha stika hizo leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa wiki ya mazingira ngazi ya Kampuni nchini kote ambapo kauli mbiu yao ni Fikiri kabla ya kula: hifadhi mazingira kwa uchukuzi endelevu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Reli Tanzania( TRL) Severine Kaombwe akishiriki zoezi la kusafisha maeneo ya Stesheni ya Dar es salaam leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa wiki ya mazingira ngazi ya Kampuni nchini kote ambapo kauli mbiu yao ni Fikiri kabla ya kula: hifadhi mazingira kwa uchukuzi endelevu.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Reli Tanzania wakimpongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Reli Tanzania( TRL) Severine Kaombwe(hayupo katika picha) leo jijini Dar es salaam mara baada ya uzinduzi wa wiki ya mazingira kwa ngazi ya Kampuni hiyo.Picha na MAELEZO_Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad