HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 21, 2013

Mh. January Makamba kuwa mgeni rasmi Redd's Miss Tanga 2013

NAIBU Waziri wa Sayansi na Tekinolojia January Makamba,anatarajia kuwa mgeni rasmi, katika shindano la umsaka malikia wa Redd's Miss Tanga 2013 linalotimua vumbi katika uwana wa Mkwakwani Mkoani hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Mkurugenzi wa DATK Intertainment Asha Kigundula alisema, maandalizi yamekamilika kilichosalia ni muda kufika na mrembo kuwekwa hadharani.

“Nashukuru mungu mambo yameenda sawa, kilichokuwa kimesalia ni kumtangaza mgeni rasm na nashuuru tumeisha mpata tayari mh;Makamba na hakuna kingine, cha muhimu mungu atuongoze katika shughuli yetu esho mambo yaende sawa,”alisema Kigundula.

Aidha Kigundula alisema, ameamua kutoa zawadi ya fedha taslimu kwa warembo na sio vitu ili warembo wake waweze upata fursa ya ujichagulia kitu cha kununua wenyewe uliko ununuliwa na kudai uwa mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha sh 500,000, wa pili sh 300,000 na wa tatu sh 250, 000.

Huku wa nne na tano wakipata sh.200, 000 kila mmoja na warembo wengine watakaosalia watapata kitita cha sh 100,000 kila mmoa kama kifuta jasho pamoja na zawadi kwa mrembo mwenye nidhamu ili kuweza kuboresha shindano hilo.

Kigundula alisema, kwa upande wa Burudani msanii wa kizazi kipya, Tunda Man, ataongoza safu ya burudani, ambapo itakuwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Dr John, Nabisha kutoka kundi la THT, Fady Dady na wasanii chipukizi kutoka mkoani hapa.

Kigundula alisema shindano hilo linatarajiwa kuanza majira ya saa mbili usiku na kushirikisha warembo 12 ambao watachuana ili kuweza kumpata malkia wa mkoa huu ambaye atauwakilisha mkoa katika mashindano hayo ngazi ya kanda.

Warembo hao ni Hawa Ramadhani (18),Hazina Mbaga (19)Like Abdulraman (19), Irene Thomas(20), Tatu Athumani (19), Winfrida Gutram (21)Lulu Mbonela (19) ,Hazina Daniel (19),Lulu Matawalo(22),Judithi Moleli (21),Neema Jonas na Hawa Twaybu(21).

Aliongeza wa kuwataka wakazi wa Tanga na Mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kushuhudia shindano hilo la aina yake, ambalo litajenga historia mypa kwa Mkoa huu, Shindano la Redds Miss Tanga 2013 limedhaminiwa na  Redds, Miss Tanga, imedhaminiwa na Al Hayat Investment Limited, Dodoma Wine, CXC Africa,Executive Solutions,Busta General Supply, Mkwabi Interprises,Lusindic Investment LTD, Lavida Pub,Jambo Leo,Staa Spoti,Five Brothers Cloud's Media Group, pamoja na Blog Michuzi Media Group,Bongostaz.com, Saluti5,Kajuna, JaneJohn, na Kidevu na assengaoscar.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad