HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 29, 2013

MATUKIO MBALI MBALI YA JENGO LILILOPOROMOKA LEO JIJINI DAR

Jengo lililo pembeni mwa msikiti wa Shia Ithnaasheri mtaa wa Indira Ghandi katikati ya jiji la Dar es salaam linavyoonekana baada ya kuporomoka asubuhi hii. Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es salaam Suleiman Kova kawaambia wanahabari kuwa kila aliyehusika na ujenzi, usimamizi na hata utoaji vibali atawajibishwa endapo kutaonekana kumekuwepo uzembe upande wake
Watu wengi wakiwemo ndugu wa watu waliokuwepo kwenye jengo hilo wakiangalia hata ya kuokolewa kwa ndugu zao.
Juhudi za uokoaji zikiendelea japo kuna uhaba mkubwa sana wa vifaa vya uokoaji.
 wananchi wakishuhuria kwa huzuni
Moja ya Magreda yaliopo eneo hilo la tukio likiendelea na kazi  ya kutoa kifusi ili kurahisisha kazi ya uokoaji.
Kikukweli hali bado ni tete katika uokoani,maaka pia kuna ufinyu wa nafasi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick akiwasili eneo la tukio ili kuungana na waokoaji wengine kwenye zoezi hilo.
Watu wanajitahidi kwenye uokoani,lakini kuna uhaba wa vifaa vya uokoaji.
Mkuu wa Mkoa akisogea eneo la tukio.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Mh. Said Meck Sadick akipatiwa maelezo ya namna ya uokoaji kutoka kwa maafisa wa kikosi cha Uokoaji.
Wanajitahidi lakini wanakwamishwa na vifaa.
Wadau wakionyesha nondo zilizokuwa zimejengewa kwenye jengo hilo wakimaanisha kuwa hazina ubora.
Magari yaliyokuwepo jirani na jengo hilo yakiwa yameangukiwa na kifusi.
Kazi ikiendelea huku wengine wakiwa hawaani kilichotokea.
Mawasiliano ya hapa na pale yakiendelea kuhakikisha utaratibu wa uokoaji unafanikiwa.


Kikosi ya Msalaba mwekundu kipo eneo la tukio.
Ulinzi mkali.
Mdau akiwahisha ngazi kwa ajili ya kuendeleza zoezi zima la uokoaji.

Mpiga picha wa Magazeti ya Serikali ya Daily & Sunday News na Habari leo,Mohamed Mambo akiwajibika kuhakikisha anapata picha bora.
Kumbukumbu ikichukuliwa.


Mh. James Mbatia akijadiliana jambo na mmoja wa wadau walipo eneo la tukio.

3 comments:

  1. inasikitasha, mainjinia wawe makini sana na vipimo kabla ya ujenz, wasikurupuke 2.

    ReplyDelete
  2. hata bado kila mkijidai wajanja na akili nyingi ndio mtakavyokufa kwa wingi rushwa itawamaliza

    ReplyDelete

Post Bottom Ad