HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 14, 2013

WANAFUNZI IFM WAVAMIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI NI BAADA YA KUKOSA ULINZI KWENYE HOSTELI, BAADA YA WENZAO WAKIUME WAWILI KUBAKWA NA MAJAMBAZI NA KULAZWA HOSPITALI. SAKATA LINAENDELEA KIGAMBONI MIDA HII CHINI YA USIMAMIZI WA KAMANDA KOVA

Wanafunzi wa Chuop Cha Uongozi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wakiwa mbele ya geti la Wizara ya Mambo ya ndani walipovamia leo majira ya saa nne nanusu asubuhi wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya Hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara. Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndio siku waliovamiwa wenzao wawili wakiume na kubakwa  hali iliyosababishwa wanafunzi hao kubakwa. Majambazi hao wamekua wakidai kupewa Laptop simu na fedha kama mwanafunzi akikataa humfanyia vitendo vya kulawiti.
Ulinzi uliimarishwa nnje ya jengo la Wizara ya Mambo ya ndani kufuatia kadhia hiyo ya wanafunzi.
Kamanda wa Polisi wa Kanda maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova akimsikiliza Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha IFM mara baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane waende hadi Kigamboni kwenye Kituo walichoripoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao. Kova aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita.
"Wanafunzi wenzetu wa kiume wamelawitiwa nyinyi tumewapa taarifa siku ya ijumaa kuwa hatunaulinzi tunaibiwa hovyo vitu vyetu halafu siku hiyo hiyo unafanyika ubakaji huo"
Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mitaa ya Posta jijini humo wakielekea kwenye kivuko cha Kigamboni ili kwenda kumuonyesha Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova.
Wakianza maandamano kuelekea Feli kwaajili ya kuvuka kwenda Kigamboni.
Kova akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya hatua zitakazochukuuliwa baada ya kupata taarifa hizo ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wote kwapamoja kwenda Kigamboni kufuatilia tukio hilo kwa pamoja.
Mitaani Posta.
Hadi kieleweke!
Tunaimba! Tunavuka bure Tunavuka bure kwenye Pantoni.
Kova akishangiliwa wakati wa safari kuelekea Feli.
Kwenye Kona ya feli kuwania geti ili waingie bure!
Wakajazana kupita kiasdi Kova akazuia kivuko kisiondoke hadi wapungue!
Hapa wakigoma kupungua kazi iliyochukua zaidi ya Saa moja hadi kivuko kuendelea na kazi ya kuvusha abiria
Pamoja na kutakiwa kupungua hapa wengine walizidi kuendelea kuingia na kukijaza kivuko hicho. hii ni sehemu ya kwanza tutawaletea sehemu ya pili ya tukio hili ambalo hadi hivi sasa filamu inaendelea hapa feli na ikielekea Kigamboni.

11 comments:

  1. Tunatumia kodi zetu kusomesha majambazi ona sasa!
    Hivi mpaka vurugu ndio watu wafanye kazi???

    ReplyDelete
  2. that is why people question about our standard of education.. Just imagine these are the so called WASOMI wa nchi hii! But they cannot even figure out what danger is facing them just a second the ferry leave the gate... Munajidhalilisha na kulidhalilisha taifa. Be sensible kuonyesha usomi wenu.

    ReplyDelete
  3. Huu ni upumbavu, halafu wakizama watailaumu serikali...huu usomi mwingine bwana. kwani ukiwa na madai ndo hutumii akili yako?

    ReplyDelete
  4. Yani maoni yote mawili yana maana kubwa,sihitaji kuongeza chochote,hao ni wahuni si wasomi kama ni wasomi wa viongozi wao tatizo la tanzania kila kitu siku hizi ni siasa utaona chadema kesho imekuwa shughuli yao,kazi kweli?kweli?

    ReplyDelete
  5. hivi ungekuwa wewe umeingiliwa kinyume ungefanyeje?

    ReplyDelete
  6. Hayajawakuta ndo maana mnachukulia jambo kiurahisi,tafakari kabla ya kucoment co kukurupuka (can you imagine mwanao wa kiume analawitiwa hasa kipindi hiki kigumu cha kuanza exams) unamcomfuse mind yake,ucfikiri wao wanapenda kuishi huko wamevumilia mengi sana sasa imefikia kikomo.jst an advice.

    ReplyDelete
  7. wanachodai ni haki. kwanini tusubiri mpaka watu waandamane ndiyo twende tukafuatilie???. matukio yote yamekuwa yakiripotiwa bila hatua kuchukuliwa. sasa wanafunzi wamekosa nini?? anayewaponda hawa vijana ana matatizo

    ReplyDelete
  8. Nyie anony wawili mnakosoa hao wanafunzi wakati hamjui hata kilichotokea au huo ndio usomi wenu sasa, bure kabisa, mngejijuza kilichotokea msingesema hizo blah blah zenu!

    ReplyDelete
  9. Nyinyi kwa sababu mlisoma bure au mlisoma mkiwa hampati shida ndio maana mwaweza tamka kuwa mnalipa kodi zenu kusomesha majambazi hamijui kadhia wanayopata wanafunzi hao better keep your mouth shut maana mtakuja kulaumu polisi mara baada ya kusikia wamebakwa hadi kufa sasa sijui ndo mtafurahi? wana haki ya msingi kudai kile kilichokuwa cha haki kwao.

    ReplyDelete
  10. Mbona watu wanaangalia matokeo tu hawaangalii sababu na kisa na mkasa?ebu fikiria mtoto wako au ndugu yako au rafiki yako au mume au mke wako anasoma IFM na kukaa hosteli. Na hosteli wanavamiwa na waharifu na kunyang'anywa laptop na simu tena sio mara mmoja.Pamoja na kuripoti kwa polisi na hao wezi kueleweka bado wanaendeleza uharifu na kufikia hatua ya kubakwa na kulawitiwa.
    Hivi wewe ukilawitiwa pamoja na kuripoti mara kadhaa polisi hauta andamana? Usiringanishe na wasomi ambao wanamazingira mazuri ya kuishi na kusoma,hawa ni walalahoi ambao jeshi la polisi limeshindwa kuwahakikishia ulinzi na usalama wao kwa kupuuzia.
    Ebu angalia suala la kubakwa na kulawitiwa linavyochukuliwa kurahisi rahisi ivi mnajua madhara yake kisaikolojia yalivyo?
    Mpaka Kova anaingilia inaamaana mkuu wa polisi kule kigamboni na Ilala wameshindwa kazi ya vibaka?
    Jeshi halina maadili sasa,hata mimi niliwahi kuporwa zamani Kigamboni na nikatoa taharifa,pamoja na polisi kujua waharifu hao hakuna kilichofanyika.
    Jeshi la polisi la Tanzania ni makini na likitaka kufanyia kazi uharifu wowote Tanzania linaweza tena kwa masaa machache tu trust me. Tatizo maadili hakuna kila kitu lazima lazima kuwe na maslahi,mimi niliombwa pesa za kufanikisha zoezi.

    ReplyDelete
  11. Polisi wa kituo cha kigamboni ni balaa, ukienda kuripoti tukio la ujambazi unaweza kaa masaa 5 bila kupewa ushirikiano wowote. Mimi siku moja nimeibiwa nikienda kuripoti pale nilikaa masaa matano naambiwa mpelelezi hajafika alipofika kaanza kunywa chai kwa kujivuta mpaka niliamua kuondoka na kuacha na hiyo kesi. Kwa kweli ushirikiano wao zero.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad