HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 6, 2012

Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2012 waanza ziara mikoani

 Hili ndilo Basi la Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2012 ambao wapo kwenye ziara ya kutembelea mikoa ya Kanda ya Kaskazini.

JUMLA ya warembo 29 kati ya 30 wanaowania taji la REDDS MISS TANZANIA 2012 leo wameanza rasmi ziara ya kutembelea Vivutio mbali mbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini ambayo ni Moshi, Arusha na Manyara. 

 Warembo hao wakiongozwa na Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania, wakiwa katika mikoa hiyo watatembelea vivutio hivyo na kuhamasisha jamii ya watanzania kuwa na desturi ya kutembelea vivutio hivyo vya ndani na kuhamasisha utalii. 

 Pia warembo hao watapata fursa ya kujifunza vitu mbalimbali kuhusiana na masuala ya utalii. Oktoba 7, warembo hao watatembrelea Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, katika lango kuu la kupandia Mlima huo la Marangu. 

 Aidha kwa mujibu wa ratiba hiyo, inaonesha kuwa warembo hao watafanya tamasha la Michezo mjini Arusha kabla ya kuelekea Monduli ambako Oktoba 8 watazuru Kaburi la Waziri Mkuu wa Zamani, Hayati Edward Moringe Sokoine.
 Baadhi wa warembo wa Redd's Miss Tanzania wakiwa ndani ya Basi wakiangalia bidhaa mbali mbali zinazouzwa na Wamachinga wa eneo la Chalinze.
 Mapumziko ya Chakula cha Mchana katika Mgahawa wa Highway,Wilayani Korongwe mkoani Tanga mchana wa leo.
 Wakielekea kwenye msosi.
 Katika Pozz tofauti tofauti. 
Mrembo Fatma Ramadhan akionyesha sehemu ya vipaji alivyonavyo ambapo amesema kimoja wapo ni kushika kamera na kupiga picha.
 Wakati wa Msosi.
Warembo wakiwa ndani ya basi lao huku safari ikiendelea.
 Chombo kikiteremka Wami.
 Eneo la Mkata.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad