Friday, August 31, 2012

Uzinduzi wa Kinywaji cha Maltiza jijini Arusha leo

 Balozi wa Kinyaji kipya kisicho na kilevi cha Maltiza ambacho kinatengenezwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Sophia Amein (kulia) akimpa kinywaji hicho mmoja wa wakazi wa jiji la Arusha ili akionje wakati wa uzinduzi wake uliofanyika jioni ya leo katika viwanja vya Sanawari,jijini Arusha.
 wakazi wa jiji la Arusha wakiwa wamejitokeza kwa wingi ili wakionje kinywaji kipya cha Maltiza ambacho hakina kilevi wakati wa uzinduzi wake uliofanyika jioni ya leo katika viwanja vya Sanawari,jijini hapa.
Wasanii wa Kikundi cha Hakuna Matata cha jijini Arusha wakitembeza mfano wa Kinywaji kipya cha Maltiza ambacho hakina kilevi kinachotengenezwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa watu mbali mbali waliofika kwenye uzinduzi wake uliofanyika jioni ya leo katika viwanja vya Sanawari,Jijini Arusha.
Kikundi cha Maonyesho ya Sanaa ya Sarakasi kifahamikacho kwa jina la Hakuna Matata chenye maskani yake jijini Arusha kikifanya Maonyesho katika viwanja vya Sanawari,jijini Arusha wakati wa Uzinduzi wa Kinywaji cha Maltiza jioni ya leo.
Mmoja wa mabalozi wa Maltiza,Lyidia Joseph akiruka kamba sambamba na Wasanii wa Kikundi cha Hakuna Matata.
Mabalozi wa Kinywaji cha Maltiza wakionyesha umahiri wao wa kulisakata dansi wakati wa Uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika jioni ya leo katika viwanja vya Sanawari,jijini Arusha na kuhudhulia na mamia ya wakazi wa Jiji la Arusha.
Mdau kutoka TBL akionja kinywaji hicho.
Mamia ya wakazi wa Jiji la Arusha wakiwa wamefurika katika viwanja vya Sanawari kushuhudia uzinduzi wa Kinywaji kipya na kisicho na kilevi cha Maltiza.

No comments:

Post a Comment