HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 14, 2012

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii yatembelea NHIF jijini Dar leo

 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Dk. Faustine Ndungulile akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo na viongozi wakuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakati kamati yake ilipofanya ziara katika makao makuu ya Shirika hilo yaliyopo Kurasini,jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Mh. Deogratius Mtukamazina  (kulia) akitoa salamu ya Bodi yake kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii iliyofanya ziara yale leo kwenye makao makuu ya Mfuko huo yenye lengo la kujifunza mambo mbali mbali yanayofanya na Mfuko huo.Wengine pichani ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Dk. Faustine Ndungulile,Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Mh. Dk. Hussein Mwinyi,Naibu Waziri wa Afya, Dk. Sirra Umbwa,Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI),Mh. Majaliwa K. Majaliwa.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Mh. Dk. Hussein Mwinyi akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii iliyofanya ziara yale leo kwenye makao makuu ya Mfuko huo yenye lengo la kujifunza mambo mbali mbali yanayofanya na Mfuko huo.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini,Mh. Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu akisalimia wadau.
Mjumbe wa Kamati hiyo na Mbunge wa Jimbo la Nzega, Dk. Hamisi Kigwangalla nae akisalimia wadau.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Ndg. Emmanuel Humba akitoa maelezo mafupi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii wakifuatia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa ukumbini hapo.
Wakurugenzi wa NHIF.
Wajumbe wa Bodi ya NHIF.
Meneja wa Idara ya Uanachama wa NHIF,Bi. Ellentruder Mbogoro akielekeza jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii walipotembelea makao makuu ya Mfuko huo,Kurasini jijini Dar es Salaam leo.
Afisa Nyaraka wa NHIF,Erastus Msigwa akiwaonyesha Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii moja ya mafaili ya Wanachama wa Mfuko huo yaliyohifadhiwa kwenye Masanduku ya Kisasa yanayotumia mfumo wa Umeme.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii wakipata maelezo ya namna ya uhifadhi wa Nyaraka kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Sehemu ya Masanduku hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad