HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 9, 2012

GRAND MALT YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA TUZO ZA EXCEL WITH GRAND MALT MKOANI DODOMA JIONI YA LEO

Washindi wa tuzo za Excel With Grand Malt kutoka Vyuo vya CBE na UDOM wakiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi wa Vyuo hivyo,Wafanyakazi wa kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL) na Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini huku wakionyesha fedha zao walizoshinda mara baada kukabidhiwa jioni ya leo kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma.
Mmoja wa Washindi wa Tuzo za Excel With Grand Malt kutoka chuo cha CBE Mkoani Dodoma akionyesha zawadi ya fedha taslim alizokabidhiwa baada ya kuibuka kidedea katika Shindano hilo ambalo kilele chake kimefanyika leo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma (U-Dom) jioni ya leo.Wengine Pichani toka kushoto ni Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt,Consolata Adam,Mshauri wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma,Ndugu Manongi,Pamoja na Mgeni rasmi katika shughuli hiyo ambaye ni Muwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.
Mmoja wa Washindi wa Tuzo za Excel With Grand Malt kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (kulia) akihakikisha fedha za zawadi alizokabidhiwa baada ya kuibuka kidedea katika Shindano hilo ambalo kilele chake kimefanyika leo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma (U-Dom) jioni ya leo.
Mdau Josephat Lukaza ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma akipokea zawadi yake ya ushindi wa  tatu katika kipendele cha Mazingira kwenye shindano la Excel With Grand Malt kwa vyuo lililokuwa likiendeshwa na kampuni ya bia tanzania kupitia kinywaji chake kisicho na kilevi cha Grand Malt.
Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt,Consolata Adam akizungumza wakati wa fainali za Mashindano ya Excel With Grand Malt zilizofanyika jioni ya leo kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma.
Waziri wa Serikali ya Wanafinzi wa CBE Dodoma (katikati) akipokea cheti cha Shukrani kutoka kwa Mgeni Rasmi.
Mshauri wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma,Ndugu Manongi (katikati) akipokea cheti cha Shukrani kutoka kwa Mgeni Rasmi.
Mkali wa Muziki wa Bongo Fleva,Joseph Haule a.k.a Prof. Jay wa Mitulinga akiwapagawisha mashabiki wake jioni ya leo mara baada ya kumalizika kwa shughuli ya ugawaji wa vyeti wa washindi wa shindano la Excel With Grand Malt.
Furaha ya ushindi chuoni hapa.
Maandalizi ya kushangilia.
Katika fainali hizi michezo mbali mbali ilikuwepo,kama huu mchezo wa Voleyball kwa timu za Chuo cha Dodoma
Kuvuta kamba.
Kuruka kwa Magunia.
Mdau Victor wa Intergrated akiselebuka sambamba na mshindi wa mbio za magunia.
Mchezo wa Netball.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad