Wednesday, February 29, 2012

Taifa Stars yatoka sare ya bao 1-1 na msumbiji leo

Mshambuliaji wa Taifa Stars, Mrisho Ngasa (kushoto) akichuana na beki wa Msumbiji, Almiro Lobo katika mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Nahodha wa Timu ya Taifa (Taifa Stars),Shadrack Nsajigwa akiwatoka mabeki wa timu ya Taifa ya Msumbiji (Mambas) katika mchezo uliopigwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wa kuwania tiketi ya kufuzu kucheza Mataifa ya Afrika 2013 nchini yatakayofanyika nchini Afrika Kusini.Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.
Golikipa wa timu ya taifa ya Msumbiji, Joao Raphael akiwa chini huku mshambuliaji wa Stars, John Boko akikosa bao la wazi baada ya kubaki yeye na kipa tu langoni.
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa Stars, Vincet Barnabas akimtoka Beki wa Timu ya Taifa ya Msumbiji,Stelio Ernesto.
Mwinyi Kazimoto akishangilia bao aliloifungia Stars na kuyafanya matokeo ya mechi hiyo kuwa 1-1
Kocha wa Stars Jan Poulsen (kulia) akipeana mkono na Kocha wa Msumbiji, Gert Angels mara baada ya mpira kumalizika.

Na Francis Dande

Timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars, leo imeshimdwa kutamba mbele ya timu ya Taifa ya Msumbiji 'Mamba's kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya kutoka sare ya 1-1 katika pambano la kuwania kufuzu Mataifa Afrika 2013 nchini Afrika Kusini.

Wiki moja iliyopita, Taifa Stars iliambulia sare ya 0-0 dhidi ya DRC katika mechi ya kujipima nguvu, huku gonjwa sugu la kufumania nyavu likionekana kushindwa kutafutiwa ufumbuzi na Poulsen kiasi cha kukigharimu kikosi hicho leo. 

Pambano hilo lililopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam lilikuwa ni la kwanza kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Mataifa Afrika 2013 nchini Afrika Kusini, ambapo Stars imetoka sare ya bao 1-1 na Msumbiji. 

Stars iliyoingia dimbani ikitoka kuchagizwa na wakali kadhaa walioiwezesha Tanzania kufuzu fainali za mwaka 1980, ilionekana dhahiri kutokuwa katika mfumo wa kuweza kuibuka wababe, ikimtumia mshambuliaji mmoja John Boco ambaye alikosa mabao ya wazi.

Pambano lilianza kwa muendelezo wa kosakosa miongoni mwa safu ya mbele ya Stars, ambako dakika ya 15, John Boko alikosa bao, kabla ya kipa wa Stars Juma Kaseja kuokoa shuti la Clesio Bauque aliyekuwa mwiba katika safu ya ulinzi. Bao la Msumbiji lilifungwa na Clesio Bauque dakika ya 22, baada ya kuwatoka mabeki wa Stars kumpoteza Juma Kaseja langoni, kabla ya Mwinyi Kazimoto kusawazisha dakika ya 40. 

Kazimoto alifunga bao hilo kwa shuti la nje ya boksi, akimalizia pasi safi ya Vicent Barnabas. Hadi mwamuzi Moahammed Farouk Misri anapuliza filimbi ya mapumziko, timu zilikuwa sare kwa bao 1-1. 

Kipindi cha pili licha ya Stars kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Nozar Khalfan, Abdi Kasim na Vicent Barnabas na kuwaingiza Mrisho Ngasa, Salum Aboubakar na Husein Javu, bado iliendelea kukosa mabao kiashi cha Boco kuzomewa na pambano kumalizika kwa sare hiyo inayoweka shakani nafasi ya Tanzania kusonga mbele.

Taifa Stars: Juma Kaseja, Shadrack Nsajigwa, Stepheno Mwasyika, Juma Nyoso, Aggrey Morris, Shabani Nditi, Nizar Khalfan, Mwinyi Kazimoto, John Bocco, Abdi Kassim ‘Babi’ na Vincent Barnabas.

Msumbiji: Joao Raphael, Edson Sitoe, Zainadine Junior, Eduardo Jumisse, Jerenias Sitoe, Elias Pelembe, Clesio Bauque, Francisco Muchanga, Stelio Ernesto, Francisco Massinga na Almiro Mohammed.

2/29/2012 ~ Copyright: Othman Michuzi ~ Mtumie Rafiki Yako , Maoni: 0

President Kikwete launching the Presidential Award on the Extractive Industry Corporate Social Responsibility and Empowerment Programme (CSRE) last night.

President Jakaya Mrisho Kikwete speaks last night at the launching ceremony of the Presidential Award on the Extractive Industry Corporate Social Responsibility and Empowerment held at the Kilimanjaro Hyatt Regency hotel in Dar es salaam.
President Jakaya Mrisho kikwete greets the chairman of Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative (TEITI), Judge Mark Bomani (rtd) last night at the launching ceremony of the Presidential Award on the Extractive Industry Corporate Social Responsibility and Empowerment held at the Kilimanjaro Hyatt Regency hotel in Dar es salaam. Looking on is ambassador Juma Mwapachu.
President Jakaya Mrisho Kikwete arrives last night at the launching ceremony of the Presidential Award on the Extractive Industry Corporate Social Responsibility and Empowerment held at the Kilimanjaro Hyatt Regency hotel in Dar es salaam. Right is the Minister for minerals and Energy Mr William Ngeleja and left is the Dar es salaam Regional Commissioner,Mr. Said Meck Sadick.
President Jakaya Mrisho Kikwete arrives last night at the launching ceremony of the Presidential Award on the Extractive Industry Corporate Social Responsibility and Empowerment held at the Kilimanjaro Hyatt Regency hotel in Dar es salaam. Right is the British High Commissioner to Tanzania Ms Diane-Louise Corner, second left is the Minister for minerals and Energy Mr William Ngeleja and far left is the Dar es salaam Regional Commissioner,Mr.Said Meck Sadick.

2/29/2012 ~ Copyright: Othman Michuzi ~ Mtumie Rafiki Yako , Maoni: 0

Mwamvita Makamba Akabidhi mikopo nafuu kwa vikundi tisa vya Mirerani

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,akiongea na wakina mama wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani  Manyara, mara alipofika kijijini hapo kutoa mikopo ya kifedha kwa vikundi mbalimbali vya kinamama,ambapo urudishwa kwa njia ya m-pesa bila riba,Mikopo hiyo huendeshwa na Mfuko wa kampuni hiyo MWEI kupitia Vodacom Foundation,zaidi ya kinamama 108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki saba,(9,700,000).
Bi.Johari Mwaselela wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,akisaini nyaraka za kupewa mkopo wakati Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,wapili toka kulia alipofika kijijini hapo kutoa mikopo ya kifedha kwa vikundi mbalimbali vya kinamama,Huduma hiyo ya Mikopo hutolewa na Vodacom Foundation kupitia mradi wake wa kusaidia wakinama MWEI na kurudishwa kwa njia ya m-pesa bila riba,zaidi ya kinamama 108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki saba,(9,700,000)kulia ni Afisa wa Mradi huyo Ally Mbuyu,na kushoto ni Meneja wa Mradi huo Mwamvua Mlangwa.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,akimshuhudia Glory Muro, wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani  Manyara,akisaini nyaraka za kupewa mkopo wa kifedha inayolenga kuwakomboa wakinamama hapa nchini, Huduma hiyo hutolewa na Vodacom Foundation kupitia mradi wake wa kusaidia kinama wa (MWEI) na kurudisha fedha hizo bila riba kwa njia ya m-pesa,zaidi ya kinamama 108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki saba,(9,700,000)kulia ni Afisa wa Mradi huo,Bw. Mbuyu.
Baadhi ya kinamama wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakifurahia jambo wakati walipokuwa wakiongea na Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,(hayupo pichani) mara alipofika kijijini hapo kutoa mikopo ya kifedha kwa vikundi mbalimbali vya kinamama,Mikopo hiyo urudishwa kwa njia ya m-pesa bila riba,Huduma hiyo hutolewa na Vodacom Foundation kupitia Mradi wa MWEI,zaidi ya kinamama 108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki saba,(9,700,000).
Baadhi ya kinamama wa Kijiji cha Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa kwenye picha ya pamoja na Ofisa Mkuu na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,wanne toka kushoto na Meneja wa Mradi wa MWEI Mwamvua Mlangwa mara baada ya kufika hapo kutoa mikopo ya kifedha kwa vikundi mbalimbali vya kinamama kijijini hapo,Mikopo hiyo urudishwa bila riba kwa njia ya m-pesa,Huduma hiyo hutolewa na Vodacom Foundation kwa kupitia Mradi wao wa MWEI,zaidi ya kinamama 108 walifaidika na Mkopo huo wa kiasi cha Shilingi Milioni tisa na laki saba,(9,700,000).

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Bi. Mwamvita Makamba amewataka wanawake wajasiriamali hususan wadogo kutambua kuwa maendeleo ya biashara zao na hatimae hali zao za kiuchumi kutategemea pamoja na mambo mengine namna wanavyotumia vizuri fursa za uwezeshaji wanazotengenezewa.

Bi. Mwamvita ametoa changamoto hiyo Wilayani Simanajiro, Mkoani Manyara katika kijiji Cha Mirerani wakati akikabidhi mikopo isiyo na riba wala dhamana yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni Tisa kwa vikundi tisa vya akina mama iliyotolewas na mradi wa Vodacom wa kusaidia wajasiriamali wadogo wanawake wa MWEI.

Bi. Mwamvita amesema kadiri ambavyo wanawake watakuwa tayari kutumia vema fursa wanazotengenezewa ikiwemo ya MWEI wanajiweka katika nafasi nzuri ya kujiwezesha kiuchumi na kuondokana na dhana kwamba mwanamke ni kiumbe tegemezi.

“Wanawake wenzangu leo Vodacom inapowakabidhi mikopo isiyo na riba wala dhamana ni fursa adhimu sana kwenu, ni wajibu wenu kutumia vema fursa hii kujiinua kama ilivyokuwa wajibu wa Vodacom kuwatafuta, kuwafikia na kuwawezesha, kazi sasa ni kwenu”Alisema Bi. Mwamvita.

Bi. Mwamvita amesema kumekuwepo na kilio kikubwa cha wanawake wajasiriamali wadogo kutofikiwa kwa urahisi ama kukosa uwezo wa kukopesheka kutoka taasisi za fedha, hivyo katika kutimiza azma ya kubadili maisha ya watanzania Vodacom ilibuni mradi wa MWEI kutatua changamoto hiyo.

“Ni vigumu kupata taasisi itakayokukopesha mfnyabishara wa vitumbua, genge mchuuzi wa samaki, msusi n.k tena bila riba wala dhamana na zaidi kukupatia mafunzo ya ujasiriamali kwa gharama zake, Vodacom licha ya kwamba biashara yetu ni huduma za simu imethubutu kubuni mradi wa mikopo kwa kuwa inapenda kuona maisha ya watanzania wakiwemo akina mama yanabadilika”Aliongeza Mwamvita
Aidha Bi. Mwamvita amewataka wanawake hao kuhakikisha mikopo waliyoichukua inleta tija katika biashara zao hasa kuinua mitaji ili nao waweze kusimama na kusaidia wanawake wengine.

“Kabla ya kuwakibidhi mikopo hii tumewapatia mafunzo ya ujasiriamali ikiwemo somo la utunzaji wa mahesabu ya biashara, tutumie elimu hiyo na mikopo hii kujiimarisha ili kuinua sauti zetu kwenye jamii”Aliongeza Mwamvita huku akisindikizwa na vigelegele vya furaha kutoka kwa akina mama.

Mradi wa MWEI ni mahsusi kwa ajili ya kusaidia akina mama nchini kama mchango wa Vodacom kuunga mkono juhudi za kitaifa za kumwezesha kiuchumi mwanamke wa kitanzania na unalenga hasa wanawake wenye biashara zenye mitaji ya kati ya Sh. 5000 na 200,000.

Bi. Mwamvita amesema kuwa mradi wa MWEI umejiwekea lengo la kuwafikia wanawake wengi zaidi hususan maeneo ya vijijini ambao pamoja na kujituma katika bishara ndogondogo wanakabiliw ana uchache wa fursa za uwezeshaji.

“Ni hatua muhimu katika maisha yetu kama Vodacom kusaidia ujenzi wa ustawi wa jamii hapa nchini, tuna namna nyingi ya kubadili maisha ya watanzania kama dira yetu invyosema, MWEI ni namna mojawapo”. Alisema Mwamvita.

Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa mikopo hiyo mbali na kuishukuru Vodacom, wanufaika hao wameahidi kuitumia vizuri mikopo hiyo ili kutimiza malengo ya kibiashara waliyonayo.

“Wengi wetu hapa ni wajasiriamali wadogo tunaojishughulisha na biashara za ususi, mama lishe n.k changamoto kubwa tuliyokuwa tukikabiliana nayo ni kuweza kufikiwa na mikopo nafuu, leo tunafuraha kuona tumepata mikopo isiyo na riba hata shilingi moja” Alisema Johari Mwaselela Mmoja wa viongozi wa Vikundi.

Amesema kupitia vikundi vyao, watahakikisha wanafanya kazi kwa pamoja na kuhimizana ili mikopo waliyopatiwa itoe tija ya kuinua mitaji yao, wakuze faida sambamba na kusaidia kubadili hali zao za maisha.

Tunawaomba Vodacom kama mlivyotufikia sisi hapa kijijini muwafikie na wenzetu wengine waliopo vijijini kama sisi na muwaokoe, kwa kweli wanawke bado tupo nyuma, tunawashukuru sana MWEI.”Aliongeza Mamam Mwaselela.

Awali Meneja wa Mradi wa MWEI Bi Mwamvua Mlangwa alisema hadi kufikia Januari mwaka huu kiasi cha Shilingi 150 Milioni kimeshatolewa na kunufaisha akina mama zaidi ya 6,000.

Bi. Mwamvua amesema idadi ya wanaohitaji mikopo hiyo ni kubwa hivyo amewasihi kina mama hao wa Mirerani kutumia vizuri fursa hiyo na kuhakikisha wanarudisha mikopo kwa wakati ili kuwafikia wanawake wa sehemu nyengine nchini.

Kupitia mradi wa MWEI Vodacom huvipatia vikundi vya akina mama mikopo pamoja na mafunzo ya ujasiriamali kazi ambayo hufanywa na Shirika la kuhudumia viwanda Vidogo – SIDO kwa gharama za Vodacom.

Mikoa ya Arusha, Manyara, Morogoro, Tanga, Rukwa na Katavi, Dodoma, Mara, Mwanza,Shinyanga na Pwani imeshanufaika na mikopo ya MWEI tangu mradi huo ulipoanzishwa mwaka 2011.

2/29/2012 ~ Copyright: Othman Michuzi ~ Mtumie Rafiki Yako , Maoni: 0

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AMALIZA ZIARA YAKE YA MKOA WA IRINGA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Iwawa baada ya kuzungumza nao wakati akimaliza ziara yake ya Wilaya ya Makete Mkoa wa Iringa jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wananchi na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Iwawa baada ya kuzungumza nao wakati akimaliza ziara yake ya Wilaya ya Makete Mkoa wa Iringa jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti cha kumiliki hisa katika Benki ya Wananchi (NJOCBA), Olive Luena, bada ya kuzindua rasmi benki hiyo iliyopo Wilaya ya Njombe mkoa wa Iringa jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti cha kumiliki hisa katika Benki ya Wananchi (NJOCOBA), Zela Edward, bada ya kuzindua rasmi benki hiyo iliyopo Wilaya ya Njombe mkoa wa Iringa jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi wa benki ya Wananchi ya (NJOCOBA) Twilumba Ulaya, baada ya kuzindua benki hiyo iliyopo Wilaya Njombe mkoa wa Iringa, jana.
Makau wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi wa Nishati katika Kiwanda cha SAO Hill, Roselyne Mariki, wakati alipowasili katika kiwanda hicho jana kwa ajili ya kuzindua mashine mpya nay a kisasa ya kuchana mbao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha SAO Hill, Nick Moore, hukusu ufanyaji kazi wa mashine mpya nay a kisasa ya kuchana mbao iliyofungwa katika kiwanda hicho, wakati alipofika kiwandani hapo jana kilichpo Wilaya ya Mafinga mkoa wa Iringa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mmoja kati ya wafanyakazi wa kiwanda cha SAO Hill, Erlend Haugen, ambaye ni mrefu kuliko wafanyakazi wote wa kiwanda hicho, baada ya kuzindua mashine cha kuchana mbao katika kiwanda hicho jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya silaha ya jadi ya kabila la Wahehe (Mkuki) kutoka kwa Mjukuu wa Chifu Mkwawa, Ignas Muyinga, baada ya kumaliza kuzindua kituo cha afya na kuwahutubia wananchi wa Kijiji cha Lungemba, Wilaya ya Mafinga mkoa wa Iringa, jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wananchi wa Kijiji cha Lungemba baada ya kuwahutubia wananchi hao, Wilaya ya Mafinga mkoa wa Iringa, jana. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

2/29/2012 ~ Copyright: Othman Michuzi ~ Mtumie Rafiki Yako , Maoni: 0

Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugombea urais 2015 - Mh. Zitto Kabwe

KABWE ZUBERI ZITTO
MBUNGE WA JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugombea urais 2015
1. Baadhi ya vyombo vya habari vimehusisha kauli yangu ya kutaka kupunguza umri wa kugombea urais na mimi ‘kuutaka urais’. Mimi nikiwa mwanachama na kiongozi wa chama chama changu cha CHADEMA naelewa na kuziheshimu taratibu na kanuni tulizojiwekea za kuomba nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo nafasi ya urais. 

Nafasi ya uongozi ndani ya CHADEMA haiombwi kwenye warsha. Iwapo chama change, wakati muafaka ukifika na kutokana na matakwa ya jamii, kikiona nipewe jukumu lolote sitasita kutekeleza wajibu huo niwe au nisiwe mgombea.

2. Kwa hivyo, nilichozungumza jana ni kutoa maoni yangu kwamba muda umefika kwa Taifa letu kupunguza umri wa kugombea urais. Maoni yangu haya yanatokana na ukweli kwamba hakuna sababu zozote za kisayansi zinazomfanya mtu aliye chini ya umri wa miaka 40 akose sifa za kuwa Rais. Msimamo huu nimekuwa nao tangu zamani nikisoma shule na haujawahi kubadilika. 

Hakuna mahala popote katika maoni yangu niliyotoa jana niliposema kwamba nataka umri wa urais upunguzwe ili nipate fursa ya kugombea nafasi ya urais. 

Pia siwezi kutaka katiba iandikwe kwa ajili yangu. Vilevile kamwe isionekane kwamba matakwa ya muda mrefu ya vijana ya kutaka umri wa kugombea Urais kupunguzwa yanalenga kunipa fursa mimi kwani mimi ni binaadamu naweza nisiwe na sifa za kuwa Rais lakini kukawa na vijana wengine wengi wenye umri chini ya miaka 40 wenye Uwezo na Uzalendo wa kutosha kushika usukani wa nchi yetu. 

Ni maoni yangu kwamba tupate mabadiliko ya vizazi katika uongozi wa nchi yetu ili kukabili changamoto za sasa zinazokabili Taifa letu.

3. Tunapojiandaa kutoa maoni kuhusu Katiba Mpya ni vizuri vyombo vya habari vikajikita kutoa taarifa bila kuweka tafsiri au kuwatafasiria maoni ambayo wananchi na viongozi watakuwa wanayatoa kuhusu maudhui ya Katiba Mpya.

Dar es Salaam
29 Februari 2012

2/29/2012 ~ Copyright: Othman Michuzi ~ Mtumie Rafiki Yako , Maoni: 0

MKURUGENZI PRECISION AIR AHIMIZA MICHEZO NA UTALII WA NDANI NCHINI

Wafanyakazi wa Precision Air walioshiriki katika mbio za Kili Marathon hivi karibuni.
Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Precision Air Patrick Ndekana akifurahia kumaliza mbio za Vodacom Fun Run.
Afisa Mawasiliano wa Precision Air Amani Nkurlu (wapili kushoto) akiwa na wafanyakazi wenzake kabla ya kuanza kwa Vodacom Fun Run.
Kaimu Mkurugenzi Patrick Ndekana akiwapongeza wafanyakazi wa Precision Air Isaac Kibuga (kushoto) na Faraji Komba (kulia) waliojishindia medali baada ya kumaliza mbio za kilomita 21.

Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la ndege la Precision Air Bw. Patrick Ndekana ametoa wito kwa watanzania kushiriki katika michezo na utalii wa ndani ili kuweza kushindana kimataifa na kujenga utamaduni wa kuenzi urithi wetu.

Akizungumza mkoani Moshi hivi karibuni kama mdhamini wa Kilimanjaro Marathon, Ndekana alisema, “Tanzania ina vipaji vingi sana katika michezo, ikiwemo riadha. Naamini kabisa kwamba wadau tukijipanga vizuri tutaweza kuibua majina makubwa wa michezo kutoka taifa hili.”

“Kwa kutambua umuhimu huu ndo maana sisi kama Precision Air tumeweza kudhamini riadha hizi kama wasafirishaji rasmi (Official Carriers) kama njia ya kusaidia na kuinua michezo nchini,” alisema Mkurugenzi huyo ambaye pia alishiriki katika mbio hizo.

“Ila lazima tuongeze munkari ya kujifunza, kukuza vipaji toka udogoni, na viongozi wa michezo wetu waweze kujitahidi kuwatafutia wachezaji wetu nafasi za kung’ara, huku sisi wadhamini pia tukitumia nafasi zetu kwa kuendelea kutoa sapoti,” alisema.

Kwa upande mwingine Ndekana alitoa pia wito kwa watanzania kujenga desturi ya kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo Mlima Kilimanjaro na mbuga mbali mbali za wanyama zilizopo nchini.

Akizungumzia umuhimu huo Bw Ndekana alisema, “Nchi yetu Tanzania ina vivutio na rasilimali nyingi sana, ikiwemo huu mlima maarufu….ingekuwa vizuri kwa sisi pamoja na watoto wetu na vizazi vijavyo kuja na kuweza kujifunza asili yetu kwa kutembelea haya maeno kuliko kuishia kuona tu katika luninga au kusoma katika vitabu.”

“Lakini pamoja na hayo hii itakuwa fursa nzuri pia kuchangia katika pato letu la taifa na kuzidi kuinua sekta yetu ya utalii nchini,” alisema Ndekana.

Bw. Ndekana pia aliwakaribisha umma kusafiri na shirika hilo la ndege kuweza kutembelea vivutio vya utalii mbali mbali nchini kwa sababu shirika hilo linasafiri karibu kila kona ya nchi ikiwemo sehemu kama Kilimanjaro, Mwanza, Zanzibar na kadhalika huku akisisitizia kuwaptia huduma bora kwa wasafiri wake.

Hii ni mara ya pili sasa kwa Precision Air kudhamini mashindano ya Kilimanjaro Marathon yanayofanyika kila mwaka Moshi, Kilimajaro. Shirika hilo ina mtandao mkubwa nchini kuliko mashirika yote Tanzania, ikiwa inafanya safari kwenda; Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Zanzibar, Mwanza, Bukoba, Kigoma, Tabora, Musoma, Shinyanga, Mtwara. Kikanda Precision Air inasafiri kwenda Nairobi, Mombasa, Entebbe, Hahaya na Johannesburg.

2/29/2012 ~ Copyright: Othman Michuzi ~ Mtumie Rafiki Yako , Maoni: 0

Dk. Shein azindua mradi wa matumizi ya teknolojia uliofadhiliwa na wamarekani

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,na Balozi wa Marekani Nchni Tanzania Alfonso Lenhardt,wakinyanyua kompyuta iliyotolewa zawdi na Balozi wa Marekani,wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Elimu wa Karne ya 21,unaohusiana na Elimu ya Teknolojia ya Habari na  mawasiliano kwa Skuli za Msingi hapa Zanzibar,unaofadhiliwa na Shrika la Misaada la Marekani USAID,uzinduzi huo ulifanyika janakatika Skuli ya Mwanakwerekwe C.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati) na Balozi wa Marekani Nchni Tanzania Alfonso Lenhardt,(katikati) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Elimu wa Karne ya 21,unaohusiana na Elimu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Skuli za Msingi hapa Zanzibar,unaofadhiliwa na Shrika la Misaada la Marekani USAID,(kulia) ni Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Wananchi,Walimu na Wanafunzi,wakati uzinduzi wa Mradi wa Elimu wa Karne ya 21,unaohusiana na Elimu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Skuli za Msingi hapa Zanzibar,unaofadhiliwa na Shrika la Misaada la Marekani USAID,katika Skuli ya Mwanakwerekwe C,(katikati)Balozi wa Marekani Nchni Tanzania Alfonso Lenhardt, na (kulia) Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Sharif.
Balozi wa Marekani Nchni Tanzania Alfonso Lenhardt,akitoa hutuba yake wakati wa ktika picha ya pamoja na Viongozi wengine na wanafunzi wakati uzinduzi wa Mradi wa Elimu wa Karne ya 21,unaohusiana na Elimu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Skuli za Msingi hapa Zanzibar,unaofadhiliwa na Shrika la Misaada la Marekani USAID,katika Skuli ya Mwanakwerekwe C.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati) akifuatana na Balozi wa Marekani Nchni Tanzania Alfonso Lenhardt,(wa pili kulia) na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad,(kulia) na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzi ya Amali Zahra Hamadi,(kushoto) alipofika katika Skuli ya Mwanakwerekwe C,kuzindua Mradi wa Elimu wa Karne ya 21,unaohusiana na Elimu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Skuli za Msingi hapa Zanzibar,unaofadhiliwa na Shrika la Misaada la Marekani USAID.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati) Balozi wa Marekani Nchni Tanzania Alfonso Lenhardt,(wa nne kushoto) Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad,wakiwa ktika picha ya pamoja na Viongozi wengine na wanafunzi wakati uzinduzi wa Mradi wa Elimu wa Karne ya 21,unaohusiana na Elimu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Skuli za Msingi hapa Zanzibar,unaofadhiliwa na Shrika la Misaada la Marekani USAID,katika Skuli ya Mwanakwerekwe C.Picha na Ramadhan Othman Ikulu.

2/29/2012 ~ Copyright: Othman Michuzi ~ Mtumie Rafiki Yako , Maoni: 0

 
Modified by MKCT
Idadi ya watu
Idadi ya watu