HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 29, 2011

Halima Mchuka wa TBC Taifa afariki dunia

MTANGAZAJI wa muda mrefu wa iliyokuwa Redio Tanzania Dar es Salaam RTD na baadae Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC),Halima Mchuka amefariki Dunia. 

Taarifa za kuaminika kabisa kutoka katika vyanzo vyetu,inaeleza kuwa  Mtangazaji huyo ambaye alikuwa na kipaji kikubwa cha utangazaji amefariki  Dunia mapema leo asubuhi wakati akiwa hospitali kutokana na kuanguka baada ya kupatwa na stroke ya gafla wakati akiwa kwenye kindindi.

Halima Mchuka inaaminika kuwa alijiunga na Radio Tanzania Dar es Salaam mwaka 1994 ambapo alifanya kazi katika idara ya Habari na idara ya mipango.

Wadau wengi wa RTD na baadae TBC-Taifa wanamkumbuka sana mama huyu wa watoto wawili kwa kuwa mwanamke wa awali kuangaza mpira katika ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki na kati.

“Unapotaja mpira wa miguu wakati huu huwezi kusahau kipindi cha michezo cha RTD cha saa mbili kasorobo na huyu dada Halima Mchuka.”alibainisha Idd Pazi mmojawapo wa wachezaji nguli wa Tanzania wa wakati huo.

Kwa hakika si wasikilizaji wa RTD na wanamichezo tu bali  hata watu wa Karibu ambao waliwahi kufanya nae kazi tunamtazama kuwa ni mtu mpole mwenye huruma na kusaidia wenzake pale penye tatizo  ambalo yeye anaweza kulitatua.

Mungu ailaze Roho ya Marehemu Halima Mchuka mahala pema peponi 

-Amina

1 comment:

  1. Poleni sana wafanyakazi wote wa TBC Taifa kwa kuondokewa na mtu muhumu sana katika Kampuni yenu, Mungu awatie nguvu ninyi pamoja na familia yake pia.
    Eee Baba yetu wa Mbinguni Mpokee Dada yetu, Mama yetu, Mpendwa wetu kwani sisi tulimpenda sana tena sana ile wewe mwenye nguvu na mamlaka umempenda zaidi Jina lako lihimidiwe Amen.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad