Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Tanzania Youth Alliance (TAYOA), Peter Masika, wakati akitazama mashine ya mawasiliano (ICT Mobile Booth), iliyotengenezwa na vijana wa TAYOA, wakati akikagua banda la maonyesho la Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) uliofanyika Geneva, Switzerland Oktoba 24, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia mfumo wa kuwasiliana kwa masafa (tele-conference) katika Banda la HUWAWEI, wakati akitembelea mabanda mbalimbali yaliyopo katika maonyesho ya ITU, jijini Geneva, Switzerland Oktoba 24, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Uhuru One, Mihayo Wilmore, kuhusu matumizi rahisi ya kompyuta ndogo na mpango wa kuzisambaza na kuwawezesha wanafunzi wa Tanzania kutumia kompyuta hizo, wakati wakati akikagua banda la maonyesho la Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) uliofanyika Geneva, Switzerland Oktoba 24, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Naibu Mkurugenzi wa Kanda (TCRA), Victor Nkya, wakati akikagua banda la maonyesho la Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) uliofanyika Geneva, Switzerland Oktoba 24, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa kuhusu Teknolojia ya mawasiliano, wakati alipotembelea Banda la maonyesho Burundi,katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) uliofanyika Geneva, Switzerland Oktoba 24, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkuu wa Mawasiliano wa Kampuni ya Qatar Assistive Technology Center, Ahmed Habib, ambaye ni mlemavu, wakati alipotembelea Banda la maonyesho la kampuni hiyo katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) uliofanyika Geneva, Switzerland Oktoba 24, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Tanzania Network Information Center, Eng. Abibu Ntahigaye, wakati akikagua banda la maonyesho la Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) uliofanyika Geneva, Switzerland Oktoba 24, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Tanzania Youth Alliance (TAYOA), Peter Masika, kuhusu namna ya kuwawezesha vijana kutumia teknolojia ya mawasiliano ya kompyuta, wakati akikagua banda la Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) uliofanyika Geneva, Switzerland Oktoba 24, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal ameiwakilisha
Tanzania katika mkutano wa ITU (International Telecommunication Union)
unaohusu wajibu nchi katika dhana ya mawasiliano unaofanyika jijini
Geneva.
Makamu wa Rais ambaye ameambatana na wadau wa masuala ya
mawasiliano kutoka Tanzania, sambamba na kushiriki kutoa mada katika
mjadala unaohusu ‘Utandawazi na Dunia kuwa kijiji’ mjadala ambao pia
umewashirikisha Balozi Philip Verveer wa Marekani, Waziri Mkuu wa
Rwanda, David Kanamugire, Naibu Waziri Mkuu wa Bahrain, Shaikh Ali Bin
Khalifa Al Khalifa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Senegal Alassane Dialy
Ndiaye na kusimamiwa na Mtangazaji wa CNN, Becky Anderson, ametumia
fursa hiyo kuuelezea ulimwengu juu ya fursa zinazotokana
na Tanzania kuwekeza katika mkongo wa intaneti chini ya bahari ya Hindi
ambao kwa kiwango kikubwa umetanua urahisi wa mawasiliano kati ya
Tanzania na nchi za Afrika Mashariki na Kusini.
Kupitia
mkongo huo, nchi jirani zitarahisisha mawasiliano yake ya Intaneti
kupitia Tanzania na taifa litanufaika na gharama za malipo kutoka katika
nchi hizo. Malawi ni moja ya nchi ambazo tayari zimeonyesha nia ya
kutaka kuunganishwa haraka.
Makamu
wa Rais pia amezungumzia ukuaji wa mtandao wa simu ambapo sasa Tanzania
kuna kadi za simu milioni 12 ambazo zimesajiliwa na kufafanua kuwa
licha ya kuwa idadi inaongezeka katika matumizi ya teknolojia, bado upo
uwanda ambao haujatumika hivyo wawekezaji wanakaribishwa sana kuwekeza
huku wakifahamu Tanzania ni nchi ya amani na yenye fursa nyingi sambamba
na kuwa na watu walio wepesi wa kupokea mabadiliko.
Tanzania
inalo banda la maonyesho hapa katika uwanja kunakofanyika mkutano huu
wa ITU, banda ambalo linasimamiwa na TCRA, sambamba na Wizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Afya ambao wanelezea namna
Tanzania inavyoweza kutoa huduma za afya kwa kutumia teknolojia ya ICT,
wahamasishaji vijana kuhusu ugonjwa wa Ukimwi TAYOA na UhuruOne ambao
wanajihusisha na utoaji huduma za kielektroniki katika shule mbalimbali
sambamba na usambazaji wa vifaa kama kompyuta.
Katika
hatua nyingine, Tanzania inaonyesha namna inavyojiandaa kuondokana na
mfumo wa urushaji matangazo sambamba na kutoa masafa kwa analojia
kuelekea digitali, hali ambayo itaongeza uhuru mkubwa kwa watumiaji
sambamba na kuwa na fursa nyingi za kupata matangazo kwa wananchi.
Mfumo
huu unahamasishwa na ITU ambayo pia katika mkutano wa mwaka huu,
inahamasisha kuhusu namna njema ya kutumia changamoto zinazotokana na
magunduzi ya Brodabendi (Broadband) mfumo unaoongeza kasi ya matangazo
ya sauti, data na video katika intaneti.
Mkutano huu wa ITU unafanyika
huku Tanzania na dunia ikiwa katika mpango wa kumaliza kabisa mfumo wa
analojia ifikapo mwaka 2015. Katika Afrika Mashariki, nchi
ya Kenya inaonekana kuongoza kufuatia kuwa tayari na sera ya kuingiza
mfumo wa
kidigitali lakini hali nchini Tanzania kwa mujibu wa TCRA iko juu na
inawezekana kabisa kuwa mfumo huo ukawa umefika maeneo yote nchini kabla
ya kuzimwa rasmi na Bodi ya dunia.
Katika
mkutano huu pia yupo Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Profesa Mbarawa Mnyaa ambaye amehudhuria mikutano kadhaa kwa ngazi ya
mawaziri huku akinadi fursa zilizopo katika wizara yake kwa wawekezaji
sambamba na kubadilishana uzoefu kuhusu makuzi ya ugunduzi katika
sayansi, teknolojia namawasiliano.
Kwa upande wake Makamu wa Rais Dkt.
Bilal pia amepata fursa ya kutembelea mabanda ya maonyesho ya nchi
jirani kama Rwanda, Kenya, Malawi, Ghana, China, Uganda na Burundi.
Katika mabanda hayo Makamu wa Rais alijionea na kupata taarifa juu ya
umuhimu wa mkongo wa Tanzania unaoziunganisha nchi za Afrika Mashariki
na Kati katika kupata huduma za Intaneti kwa gharama nafuu na pia
umuhimu wake katika kuingiza pato kwa Tanzania.
No comments:
Post a Comment