HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 13, 2011

tamasha la 10 la jinsia lafanyika jijini dar leo


Mwenyekiti wa TGNP,Mary Rusimbi akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye tamasha la 10 la jinsia,ambalo msisitizo mkuu wa tamasha hilo ni 'Jinsia,Demokrasia na Maendeleo:Ardhi,Nguvukazi na maisha endelevu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),Ussu Mallya akiwakaribisha wageni waalikwa mbali mbali asubuhi hii kwenye viwanja vya ofisi hiyo zilizopo Mabibo jijini Dar,ambako kunafanyika tamasha la 10 la jinsia,ambalo msisitizo mkuu wa tamasha hilo ni 'Jinsia,Demokrasia na Maendeleo:Ardhi,Nguvukazi na maisha endelevu.
Pichani kulia ni Mgein rasmi wa tamasha hilo kutoka nchini Ghana,Profesa Dzodzi Tsikata,akifuatia na Mwenyekiti wa TGNP,Mary Rusimbi pamoja na wanaharakati wengine wakifuatilia kwa makini yanayojiri kwenye tamasha hilo,ambali limekusanya washirirki kutoka sehemu mbalimbali,ndani na nje ya jiji la Dar.
Pichani baadhi ya wageni waalikwa na wanaharakati kutoka mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP),pamoja na FemAct wakifuatilia kwa umakini mambo mbalimbali yanayoendelea asubuhi hii kwenye tamasha hilo.
Wageni waalikwa kutoka pembezo nao wakiwa wamejumuika kwenye tamasha hilo la 10 la jinsia.
Pichani kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP,Ussu Mallya pamoja na Mwenyekiti wa mtandao huo,Mary Rusimbi wakiambatana na Mgeni rasmi wa tamasha hilokutoka nchini Ghana,Profesa Dzodzi Tsikata pichani kati na wanaharakati wengine wakiwasili kwenye tamasha hilo la 10 la jinsia asubuhi hii kwenye viunga vya ofisi hiyo,Mabibo jijini Dar.
Wageni waalikwa wakifuatia yanayojiri hivi sasa kwenye tamasha hilo la 10 la jinsia linaloratibiwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) wakishirikiana na FemAct.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad