HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 27, 2011

Mamlaka ya Elimu Tanzania yakabidhiwa Tuzo zao leo

Vikombe vya Ushindi.
Meneja wa Habari Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Siylvia Lupembe Gunze akipongezana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Rosemary Lulabuka (kulia) baada ya kumkabidhi zawadi walizoshinda kwenye Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Afrika yaliyomalizika hivi karibuni katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Rosemary Lulabuka (wa pili kushoto) akiwa na wafanyakazi wa Mamlaka wakiwa na zawadi walizopata baada ya banda lao kushika nafasi ya kwanza katika kutoa huduma bora wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyomalizika hivi karibuni.

Na Francis Dande wa Blogu ya Jamii
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) leo wamekabidhiwa zawadi mbalimbali walizopata wakati wa Maonyesho ya wiki ya Utumishi wa Umma iliyomalizika hivi karibuni katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla fupi ya kupokea zawadi hizo na kufanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Mikocheni jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi huyo aliwapongeza wafanyakazi hao kwa nidhamu ya hali ya juu waliyoionyesha wakati wote wa Maonyesho hadi kuibuka washindi wa kwanza katika kipengele cha kutoa huduma bora pamoja na banda lao kushika nafasi ya pili kwa ubora.

‘Napenda kuwapongeza sana kwa kazi nzuri na heshima na sifa nzuri mliyoipatia Mamlaka yetu tunatambua juhudi zenu na muongeze jitiada katika kazi zenu za kila siku’ alisema Mkurugenzi huyo.

Naye Meneja wa Habari Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Siylvia Lupembe Gunze alisema kuwa kujituma na kufanya kazi kwa pamoja ndio kulikowafanya kuibuka washindi katikaMaonyesho hayo yaliyozishirikisha nchi mbalimbali kutoka katika Ukanda wa Afrika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad