HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 5, 2011

video mpya ya miriam lukindo kuzinduliwa april 10 diamond jubilee

Msanii wa muziki wa injili nchini Miriam Lukindo akiwa katika pozi
Msanii wa muziki wa injili nchini Miriam Lukindo akizungumza na waandishi wa habari asubuhi hii.

MSANII wa muziki wa injili nchini Miriam Lukindo Mauki anatarajia kuzindua video ya albamu yake ya pili iitwayo "Ni asubuhi", uzinduzi huo utafanyika Aprili 10 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi hii, Miriam alisema ili kupamba uzinduzi huo wasanii mbalimbali wa muziki wa Injili watasindikiza.

Aliwataja wasanii hao kuwa ni pamoja Christina Shusho, Jackson Bent, Martha Mwaipaja, The Voice Band, The Whispers, Makuti Kawe na Marion Shako kutoka Nchini Kenya.

Nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ni pamoja na Ni asubuhi, Sema na Moyo wanghu, Anasikia,Amefanya, Wewe ni sababu, Mungu yu Mwema, Twende na Yesu na Amen Amen.

Aidha, kiingilio katika uzinduzi huo kimepangwa kuwa ni sh.10,000 kwa viti maalum na 5,000 kwa viti vya kawaida.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad