HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, April 3, 2011

TBL YAKABIDHI ZAHANATI ILIYOKARABATIWA BAADA YA KUPIGWA MABOMU GONGO LA MBOTO

Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kulia), akimkabidhi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick jengo la uzazi la Zahanati ya Kivule lililokarabatiwa na TBL baada ya kulipuliwa kwa mabomu kutoka kikosi cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) cha Gongo la Mboto, Dar es Salaam Februali 16, mwaka huu.TBL imetumia sh milioni 30 kukarabati na kununua vifaa vilivyoharibiwa.
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto), akimkabidhi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick moja ya vifaa vinavyotumika wakati wa mzazi kujifungua katika hafla ya TBL kukabidhi jengo la uzazi la Zahanati ya Kivule lililokarabatiwa na kampuni hiyo baada ya kulipuliwa kwa mabomu kutoka kikosi cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) cha Gongo la Mboto, Dar es Salaam Februali 16, mwaka huu.TBL imetumia sh milioni 30 kukarabati na kununua vifaa vilivyoharibiwa. Kulia ni Mhandisi wa Ujenzi wa TBL, John Malisa na Doris Malulu ambaye ni Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick akijaribu baiskeli ya kubebea wajawazito ambayo ni moja ya vifaa vilivyonunuliwa na Kampuni ya Bia Tanzania. Vifaa pamoja na jengo la Wazazi la Zahanati ya Kivule lililokarabatiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) vilikabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa huyo katika hafla iliyofanyika juzi. Jengo hilo liliharibiwa na milipuko ya mabomu ya Gongo la mboto iliyotokea Februali 16. Anayemsukuma ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa TBL, Steve Kilindo na Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Sophia Nkokoo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick (kushoto) akiwa na Mhandisi wa Ujenzi wa Kampuni ya bia Tanzania (TBL), John Malisa baada ya Kampuni hiyo kukabidhi Jengo la Wazazi kujifungulia la Zahanati ya Kivule lililokarabatiwa kwa msaada wa kampuni hiyo, baada ya kuharibiwa na milipuko ya mabomu ya Gongo la Mboto. TBL imetumia sh. milioni 30 kukarabati na kununua vifaa vilivyoharibiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad