HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 2, 2011

kongamalo la katika mpya chuo kikuu leo

Mwenyekiti wa Kongamano la Pili la Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr. Kitila Mkumbo (katikati) akiwa kwenye meza kuu wa watoa Mada katika Kongamano hilo ambao ni Jaji Mkuu Mstaafu,Barnabas Samata (kushoto) pamoja na Ndg. F. Kiwinga.Mada kuu ya leo ilikuwa ni Kujadili hukusu Maudhui na Misingi ya Katiba Mpya.Kongamano hili limemalizika mchana huu katika ukumbi wa Nkuruma ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Dr. Sengondo Mvungi wa NCCR-Mageuzi nae alizungumza katika Kongamano hilo lililokuwa likijadili mada ya Maudhui na Misingi ya Katiba Mpya katika nchi yetu hii.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF-Tanzania Bara,Julius Mtatiro akizungumza katika Kongamano hilo la Katiba Mpya lililomalizika mchana huu katika ukumbi wa Nkuruma,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwasisi wa Mageuzi Nchini na Mwanachama wa CHADEMA,Mabere Marando akizzungumza katika Kongamano hilo.
Kiongozi wa Chama cha UDP,John Cheyo akizungumza katika Kongamano hilo.
Mmoja wa Wadau wa Kongamano Hilo akichangia Mada zilizokuwa zikitolewa katika Kongamano hilo mchana huu.
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake nchini (TAWLA),Bi. Maria Kashonda akichangia mada zilizokuwa zikitolewa katika Kongamano hilo leo.
Viongozi wa Vyama vya Upinzani wakifuatilia Kongamano hilo.
Watu wengi walijitokeza katika Ukumbi wa Nkuruma ambapo walijaa mpaka nje ya ukumbi ili kuhakikisha mada ya Katika Mpya inajadiliwa kisawa sawa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad