HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 29, 2011

ziara ya makamu wa rais wilayani monduli leo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal katikati, akitembelea mashamba ya kilimo cha mpunga katika mabonde ya Mto wa Mbu Wilayani Monduli, wakati alipokuwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo Mkoani Arusha leo. kulia Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Isidore Shirima
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiangalia mashamba ya kilimo cha mpunga katika mabonde ya Mto wa Mbu Wilayani Munduli, alipokuwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo Mkoani Arusha leo.Picha na Amour Nassor VPO.


Na Penzi Nyamungumi - Arusha

Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal ameutaka ushirika wa wafugaji (RAMAT) wilayani Monduli kutilia mkazo ufugaji wa kisasa kwa maendeleo yao.

Dk. Bilal ametoa rai hiyo jana (Jumatatu) wakati alipokuwa akisalimiana na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi jengo la ofisi ya ushirika huo alipotembelea wilaya ya Monduli wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za maendeleo mkoani Arusha.

Aidha katika ziara hiyo Makamu wa Rais alikagua maendeleo ya ujenzi wa machinjio ya kisasa na kuona mifugo ilivyoboreshwa na vikundi vya wafugaji vinavyounda ushirika huo.

Alisema wafugaji hao wana bahati ya kuwa na machinjio ya kisasa karibu na maeneo yao ambapo watauza ng’ombe kwenye ushirika wao na kuchinjwa katika machinjio hayo na hatimaye watauza nyama kwa bei nzuri.

Alisema katika hali hiyo ya kuwa na machinjio ya kisasa hawana budi kufuga kisasa kwa kutunza mifugo yao.

“Tutie mkazo kwenye ufugaji wa kisasa ili tupate maendeleo. Tuna kiwanda cha kisasa, tutauza ng’ombe kwenye ushirika tutachinja hapa na mtapata bei nzuri,” alisema Dk. Bilal.

Aliwapongeza wafugaji hao kwa kuitikia wito wa serikali wa kutaka wananchi kujijengea misingi ya maisha bora kwa kupitia sekta ya mifugo.

Aliwataka wafugaji ambao bado hawajajiunga na ushirika huo wafanye hivyo sasa kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Taarifa ya ushirika wa wafugaji kwa Makamu wa Rais ilieleza kuwa mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi hiyo ulioanza mwaka 2009 umefikia shilingi milioni 44.8 hadi sasa sawa na asilimia 80 ya gharama zote zinazokisiwa za shilingi milioni 56.1 hadi litakapokamilika.

“Gharama za ujenzi huu inatokana na uchangiaji wa pamoja na ufadhili wa ADF (African Development Foundation) wa shilingi milioni 50.3. Vyama vya wafugaji shilingi milioni 4.5 na Mbunge wetu na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa mabati 100,” ilisema sehemu ya taarifa. 

1 comment:

  1. MWISHO WA SAFARI LAZIMA MH APITE KWA BABUUUUUUUUUUUU,

    ReplyDelete

Post Bottom Ad