HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 2, 2011

Vodacom Foundation yakabidhi madarasa kwa shule ya sokondari ya Irkisongo

Mkuu wa Wilaya ya Monduli Bw.Jowika Kasunga pamoja na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba kulia wakifunua jiwe la msingi kuashiria makabidhiano rasmi ya jengo lenye madarasa mawili yaliyojengwa kwa msaada wa Vodacom Foundation katika shule ya Sekondary ya wasichana ya Irkisongo iliyopo wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kwa thamani ya shilingi Milioni 30.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondary ya wasichana ya Irkisongo iliyopo wilaya ya Monduli Mkoani Arusha,Happiness Nyange kulia akimwelezea jambo Mkurugenzi wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba mara baada ya kukabidhi msaada wa jengo lenye madarasa mawili yenye thamani ya shilingi Milioni 30,yaliyojengwa na Vodacom Foundation.
Mkurugenzi mahusiano wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba akipongezwa na wanafunzi wa shule ya Sekondary ya Irkisongo iliyopo wilaya ya Monduli Mkoani Arusha baada ya Mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom kukabidhi msaada wa Jengo lenye madarasa mawili yenye thamani ya shilingi Milioni 30.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad