HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 5, 2011

demo-image

vurugu za maandamano ya CHADEMA zatawala mkoani arusha leo, baadhi ya viongozi washikiriwa na polisi

ISABELA+JOSEPH+100
Viongozi wa CHADEMA katika maandamano leo kabla ya kutawanywa na polisi na wengine kutiwa mbaroni
100_0036
Wanachama na wapenzi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa mji wa Arusha wakiwa wameshika mabango katika maandamano hayo kabla ya wanausalama kuanza kuzuia maandanayo hayo.
100_0042
Huyu Dogo pia nae alikuwepo katika maandamano hayo,ambapo naamini kabisa kwamba aliingia katika maandamano hayo kwa kufuata mkumbo tu.maana umri wake unaonekana ni mdogo sana.
164885_1515529300835_1612544720_1236965_5451950_n
Mke wa Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dr. Willbroad Slaa.Mama Josephine Kamili akichuruzika damu mara baada ya kutokea kwa vurugu baina ya wanachama na wapenzi wa CHADEMA dhidi ya Askari Polisi.Vurugu hizo zimezuka mchana wa leo huko mkoani Arusha mara baada ya kuzuiliwa kufanya maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanywa na chama hicho.
maandamano
Askari Polisi wakijaribu kulizuia gari moja lilikuwepo katika maandamano hayo.
polisi+wakidhibiti+waandamanaji
Wanausalama wakimtuliza mmoja wa waandamanaji aliekuwepo katika maandamano hayo.
waliopigwa+mabomu
Wakazi wa maeneo ya jirani na zilipotokea vurugu hizo wakinawa maji usoni ili kupunguza makali ya sumu za mabomu ya machozi yaliyokuwa yakilipuliwa katika kutuliza ghasia hizo.
image007
Mitaa ya Jijini Arusha ililindima milio ya Mabomu ya Machozi huku mitaa ikiwa imepoa kabisa.
image005
Askari Polisi wakiwa wameenea kila kona kuhakikisha hali inakuwa shwari na hakuna mtu anaefanya maandamano hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *