HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 9, 2010

huu ni uchakuchuaji dhahiri

hii kitu nimekutana nayo jana nilipokuwa safarini kuelekea Lushoto Mkoani Tanga,yaani basi hili linakula vichwa kama daladala za jijji la Dar.huwezi amini hawa abiria walisimama kutokea Chalinze mpaka Lushoto na wazee wa feva walikuwa wakisikamisha basi hilo na kukagua na kushuka kwa kusema "haya nawatakieni safari njema" hivi hii imekaa vyema kweli wadau.

2 comments:

  1. Kijana,
    Umenikumbusha mbali sana juu ya usafiri wa basi kati ya Dar-Lushoto maana ni viyuko vitupu. Nilikamata basi hilo Ubungo stendi ya Shamba, basi bwana, moja, aliyepokea nauli yangu hadi michungwani hata hakuwa kondakta, hivyo sikupata heshima kabisa. Mbili, hadi ninashuka michungwani karibu na kona ya Tanga, ngoma ilikuwa imejaza na nami nilishuka nikiwa bado sijapata kiti.
    Tatu, humo ndani ni kiswahili hakizungumzwi bali ni Kisambaa tu kw akwenda mbele.
    Nne, Trafiki wanalisimamisha gari na kuingia ndani na kutoka, na baada ya hapo mnaendelea na safari.
    Tano, hii ilikuwa kali zaidi, kuna jamaa aliingia katikati ya Mkata na Segera na mahindi ya mabichi ya kuuza. Mahindi hayo yalikuwa ni ya moto kama vile bado yalikuwa kwenye gae lake. Mara ghaflu basi zima kila mtu akawa anameshika hindi anatafuna. Safiri yangu katika mikoa tofauti ndani ya Tanzania, Afrika mashariki na nje ya nchi kwangu ulikuwa ni uzoefu tosha na historia ya aina yake.

    ReplyDelete
  2. Hao wazee wa Feva ndiyo chanzo kikubwa cha kuwa na ajali nyingi sana barabrani kwani hilo basi lingepata aajli tungehesabu mauti ambazo zilikuwa hazistahili kuwepo hapo.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad